• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 8:50 AM
Liverpool wakabwa koo na Newcastle United katika EPL ugani Anfield

Liverpool wakabwa koo na Newcastle United katika EPL ugani Anfield

Na MASHIRIKA

LIVERPOOL walipoteza nafasi ya kujiweka pazuri kukamilisha kampeni za Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) msimu huu ndani ya mduara wa nne-bora baada ya kuambulia sare ya 1-1 dhidi ya Newcastle United ugani Anfield mnamo Jumamosi.

Fowadi Joe Willock anayechezea Newcastle kwa mkopo kutoka Arsenal, alifuta juhudi za mshambuliaji Mohamed Salah aliyewaweka Liverpool uongozini katika dakika ya tatu. Willock alitokea benchi katika dakika ya 64 kujaza pengo la Ciaran Clark na kuwanyima wenyeji wao ushindi ambao ungewapaisha hadi nafasi ya tano.

Hata hivyo, matokeo hayo yalisaza mabingwa hao watetezi katika nafasi ya sita kwa alama 54, tano nyuma ya nambari tatu Leicester City.

Licha ya kutamalaki mchezo na kumiliki asilimia kubwa ya mpira, Liverpool wanaotiwa makali na kocha Jurgen Klopp walipoteza nafasi nyingi za wazi. Dalili zote ziliashiria kwamba wangalitia kapuni pointi tatu katika mechi hiyo baada ya goli la Callum Wilson wa Newcastle kufutiliwa mbali mwishoni mwa kipindi baada ya kubainika kwamba alikuwa amenawa mpira.

Alama moja iliyovunwa na Newcastle katika pambano hilo la jana liliwadumisha katika nafasi ya 16 kwa pointi 36, tisa nje ya mduara unaojumuisha vikosi vitatu vya mwisho – Fulham, West Bromwich Albion na Sheffield United ambao tayari wametereshwa ngazi.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

AKILIMALI: Mfumo bora kufanikisha kilimo cha matikitimaji

Uwanja wa Wembley nchini Uingereza sasa kuandaa mechi nane...