• Nairobi
  • Last Updated May 13th, 2024 6:55 AM
Liverpool yasuka njama ya kupokonya City windo la EPL

Liverpool yasuka njama ya kupokonya City windo la EPL

NA MASHIRIKA

LIVERPOOL, Uingereza

BEKI wa Liverpool, Joel Matip ameonya wachezaji wenza kabla ya siku ya mwisho ya Ligi Kuu ya Uingereza mnamo Mei 22.

Mabingwa wa zamani Liverpool maarufu kama Reds, bado wana fursa ya kutwaa taji kwa sababu wako pointi moja pekee nyuma ya viongozi Manchester City.

Inasalia mechi moja kipenga cha mwisho cha ligi ya msimu 2021-2022 kipulizwe.Vijana wa kocha Jurgen Klopp wataalika nambari nane Wolves ugani Anfield huku City wakikaribisha nambari 14 Aston Villa wanaonolewa na jagina wa Liverpool, Steven Gerrard.

Liverpool lazima wazidie maarifa Wolves na kuomba City, ambao wako chini ya kocha Pep Guardiola, wapoteze alama zote dhidi ya Villa ndiposa watwae taji.

Villa wataanza mchuano huo ugani Etihad wakiwa wanyonge.Licha ya hali ngumu wanayojipata ndani, Matip amewapa wenzake ushauri.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Cameroon amesisitiza kuwa wasiwazie kitakachokuwa kikiendelea jijini Manchester.

Matip amenukuliwa na tovuti ya klabu ya Liverpool akisema, “Kitakuwa kibarua kigumu na tusipomakinika, kitakuwa hata kibarua kigumu zaidi. Tunaweza tu kumakinikia mchezo wetu. Haitakuwa kazi rahisi dhidi ya Wolves ambao umakinifu wetu wote uko kwao. Hicho ndicho kitu pekee tunaweza kubadilisha na kitu tunafanya.”

Mzawa huyo wa Ujerumani alisema watajaribu kadri ya uwezo wao kusakata kabumbu ya kupendeza iwezekanavyo.

  • Tags

You can share this post!

Serikali kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa SGR

Wawaniaji huru tisa kumkabili ‘Jicho Pevu’

T L