• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 7:50 AM
London Marathon: Yehaulaw avunja utawala wa Kenya wa miaka sita

London Marathon: Yehaulaw avunja utawala wa Kenya wa miaka sita

Na GEOFFREY ANENE

KENYA imepoteza ubingwa wa London Marathon wa kitengo cha akina dada na utawala wa miaka sita baada ya Muethiopia Yalemzerf Yehualaw kubeba taji kwa saa 2:17:25 mjini London, Uingereza, Jumapili.

Bingwa mtetezi Joyciline Jepkosgei ameridhika na nafasi ya pili kwa 2:18:07 akifuatiwa na Alemu Megertu kutoka Ethiopia (2:18:32), mshindi wa nishani ya fedha ya Riadha za Dunia Judith Korir kutoka Kenya (2:18:43), Mromania Joan Chelimo (2:19:27), Muethiopia Ashete Bekere (2:19:30) na Mkenya Mary Wacera (2:20:22) mtawalia.

Yehualaw alichomoka hatua chache baada ya kufika katika kilomita ya 37 akiwa bega kwa bega na Jepkosgei ambaye alikosa jibu.

Kenya imepoteza ubingwa wa London Marathon wa kitengo cha akina dada na utawala wa miaka sita baada ya raia wa Ethiopia Yalemzerf Yehualaw kubeba taji kwa saa 2:17:25 jijini London, Uingereza, Jumapili, Oktoba 02, 2022. PICHA | HISANI

Kabla ya makala haya ya 42, Kenya ilikuwa imetawala makala sita mfululizo ya London Marathon katika kitengo cha wanawake kupitia kwa Jemima Sumgong (2016), Mary Keitany (2017), Vivian Cheruiyot (2018), Brigid Kosgei (2019 & 2020) na Jepkosgei (2021).

Mstaafu Keitany anashikilia rekodi ya dunia ya wanawake pekee ya 2:17:01 aliyoweka mwaka 2017.

  • Tags

You can share this post!

HUKU USWAHILINI: Ugomvi nyumbani ni burudani mtaa mzima

Montreal anayochezea Wanyama yazidi kutesa wapinzani MLS

T L