• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 10:15 PM
Madume wa Kenya wanasubiria mtihani mgumu Hoki za Afrika

Madume wa Kenya wanasubiria mtihani mgumu Hoki za Afrika

Na JOHN KIMWERE

KENYA itaingia mzigoni kukabili Misri kwenye nusu fainali ya wanaume katika magongo ya Kombe la Afrika inayoendelea ugani Theodosia Okoh Stadium, Accra Ghana.

Bila shaka madume wa Kenya waliomaliza nafasi ya pili kwenye mechi za Kundi A watarajia kibarua kigumu dhidi ya wapinzani wao. Nusu fainali ya pili itashuhudia Nigeria na wafalme wa mchezo huo barani Afrika Kusini.

Utakuwa mchezo mgumu kwa kuzingatia katuika historia ya magongo Kenya haijawahi kushinda Misri. Misri ni weledi wa kupata mabao kupitia kona.

”Tunafahamu tunatarajia kibarua kigumu mbele ya wapinzani wetu lakini tumejipanga tayari kuwakabili siki sote sio Jumapili tunajiamini tuna uwezo tosha kuwashinda ingawa hatujawahi kulemea,” naibu kocha wa wanaume, Mike Malungu alisema kupitia mtandao wa kijamii na kuongeza kuwa kamwe hawana hofu yoyote.

Pia alishukuru wachezaji wake kwa ufanisi huo licha ya kufika kwenye mashindano hayo kuchelewa. Afrika Kusini ilimaliza kileleni Kundi A kwa alama sita, tatu bele ya Kenya. Kundi B, Misri iliibuka kidedea kwa alama tisa, tatu mbele ya Nigeria.

Nao wanaume wa Kenya walikuwa wamepangwa Kundi A pia Afrika Kusini na Namibia. Wenyeji Ghana wamo Kundi B linaloshirikisha Misri, Nigeria na Uganda.

You can share this post!

Wenye ardhi waitwa serikali ikipanua barabara ya...

Vitabu vinavyotolewa na wanasiasa si vya CBC, wizara yaonya

T L