• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 4:55 PM
Majagina wamtaka Mwendwa agure FKF

Majagina wamtaka Mwendwa agure FKF

Na JOHN ASHIHUNDU

WALIOKUWA wachezaji wa kimataifa wanataka maafisa wa Shirikisho la Soka Nchini (FKF) wakae kando baada ya madai kwamba lilitumia vibaya pesa za umma.

Akizungmza kwa niaba ya majagina hao, mchezaji wa zamani wa AFC Leopards pamoja na timu ya taifa Harambee Stars, Ben Musuku, alisema kwa mujibu wa taarifa ya Waziri wa Michezo Amina Mohamed, FKF ina maswali chungu nzima ya kujibu kuhusiana na utumizi mbaya wa pesa zilizonuiwa kuimarisha kandanda nchini.

Amina alisema afisi ya Rais wa FKF, Nick Mwendwa, ilipokea zaidi ya Sh1 bilioni katika miaka mitatu iliyopita lakini haijaeleza bayana jinsi ilivyozitumia.Mwendwa amekanusha madai hayo huku akiongeza kuwwa FKF hufanyiwa ukaguzi wa hesabu za fedha kila mwaka na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).

Lakini majagina hawajaridhika na utetezi wake.“Mwendwa lazima aeleze jinsi kila shilingi ilivyotumika,’ aliongeza mshambuliaji huyo mstaafu.“(Kenya) Kupigwa marufuku (na FIFA) isiwe kisingizio. Tunachotaka kuelezwa ni jinsi pesa zilitumika,” aliongeza na kupendekeza kamati ya muda iundwe kusimamia soka nchini.

kandanda hadi uchaguzi wa wazi ufanyike.Jagina huyo alimshutumu vikali Seneta wa Nairobi Johnson Sakaja kwa kujaribu kumtetea Mwendwa kutokana na madai hayo.’Tunahitaji watu wasiokuwa na madoadoa katika uongozi wa soka ili mchezo huu uimarike,’ aliongeza.

You can share this post!

Arsenali yafululiza mechi 10 bila kushindwa

PSG, Bayern na Juve zatamba Barca ikizidi kusuasua ligini

T L