• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 12:48 PM
Makala ya michezo: Winga na nahodha ambaye ameongeza thamana kwa timu ambayo imeshiriki Ligi ya mashinani na kufuzu kwa kuwa mfungaji bora

Makala ya michezo: Winga na nahodha ambaye ameongeza thamana kwa timu ambayo imeshiriki Ligi ya mashinani na kufuzu kwa kuwa mfungaji bora

Na PATRICK KILAVUKA

Winga John Juma baada ya  kujiunga na timu yake ya sasa  DESAI FC, alipata ikicheza tu vipute.

Lakini alikuja na wazo kwamba lingekuwa jambo la busara kwa timu kujitosa katika vinganganyiro vya vigezo  vya haiba kuipa timu sura ya ukuzi na kuangazia vipaji zaidi. Na jambo hilo lilipata mashiko wakati ambapo timu ilijisajili katika Ligi ya FKF, Kauntindogo, Zoni E Nairobi West.

Kujituma kwake kama nahodha na wachezaji wenza kumejibu dau hilo kwa sababu timu imejikatia tiketi ya kushiriki katika Ligi ya Kaunti ya Shirikisho la Soka Kenya msimu ujao.Isitoshe, anaongoza ufungaji wa magoli kwa kucheka na nyavu mara 12 kwenye Ligi hiyo.

Aghalabu alikariri kwamba, akiwa shule ya upili, aliweza kumimina mabao zaidi ya 30.
Alisomea Shule ya Msingi Ya Mlima, Naitiri, Kaunti ya Bungoma kabla kujisajili Shule ya Upili ya Sirakaru ambapo aliwakisha hadi mashindano ya Kanda  katika Michezo za Shule za Upili uwanjani Kandui.

Mwanasoka wa pembeni na fowadi pia alilelewa na Mlima FC akiwa na miaka kumi na miwili kabla kunyakuliwa na Nakoba FC ambayo inacheza katika Ligi ya Kaunti ya Bungoma.
Hatimaye, kwa kutaka kusaka majani mabichi, alitua Nairobi mwaka 2020.

Winga na nahodha John Juma(wa pili kulia) kikosini mwa DESAI FC…PICHA/PATRICK KILAVUKA

Ni baada ya kutulia mjini, kiu ya kufanya mazoezi kilimsakama na aliweza kujukumika katika kikosi cha DESAI FC. Kwa vile kipawa hakifichiki, alidhibitisha uwezo wake wakati wa kujinoa na bila shaka kocha aliweza kumwaminia nafasi hiyo.

Hata alipokezwa mikoba ya ukapteni wa timu hadi sasa timu imefuzu ligini.Yeye huongoza wachezaji 34 kujinoa katika uga wa Shule ya DESAI au wanakopigia mechi za ligi uwanja wa Shule ya Msingi ya Gatina,  Kawangware.

Anasema angepaenda kufuata  nyayo za straika Henry Meja ambaye alicheza naye Shule ya Upili ya Sikararu kisha akasajiliwa na Tusker. ingava hivyo, mwanadimba Ngolo Konte wa Chelsea humtia hamu na ghamu ya kusakatia timu kubwa nchini.

Angependa shukrani zake za dhati ziwaenda wadau wa DESAI FC, kocha aliyemlea Mlima FC Moses Laisa ambaye alimgubia kwa hali na mali hadi akafaulu masomoni na kispoti na mwisho babaye Andrew Juma Sirengo ambaye alimhimiza kutokata tamaa hadi afikisha lengo la kucheza Ligi za NSL na Primia.

Mwanakabumbu Juma  anasema furaha yake ni kuona timu yake ikicheza Ligi ya Kanda hivi karibuni baada ya wachezaji kuonyesha dalili za kujituma.Ujumbe wake ni kwamba, silaha ya spoti ni kutambua kwamba asiyekubali kushindwa si mshindani bali bidii na kujituma kwawezesha mambo yote pasina na kukata tamaa!

  • Tags

You can share this post!

Kenya yapokea dozi 880,320 za chanjo aina ya Moderna

Pele afanyiwa upasuaji kuondoa uvimbe wa utumbo