• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 12:48 PM
STAA WA SPOTI: Malkia wa tenisi anayeikweza Kenya Afrika na duniani

STAA WA SPOTI: Malkia wa tenisi anayeikweza Kenya Afrika na duniani

Na GEOFFREY ANENE

ANGELLA Okutoyi ni mwanatenisi wa pekee kutoka Kenya kuwahi kutawazwa malkia wa Bara Afrika wa mashindano ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 18.

Isitoshe, Okutoyi, 17, anaendelea kuweka Kenya kwenye ramani ya dunia baada ya kuwa mchezaji wa kwanza kabisa wa kike humu nchini kuingia mduara wa wanatenisi 100-bora kwenye viwango bora vya chipukizi vya Shirikisho la Tenisi Duniani (ITF).

Amepata mafanikio hayo yote mwaka 2021.

Amezoa mataji kadhaa ya humu nchini tangu aanze tenisi akiwa katika shule ya msingi ya Loreto Convent Valley Road jijini Nairobi chini ya uangalizi wa Joe Karani na Allan Atola.

Bingwa huyo wa Kenya Open 2018 alianza mwaka 2021 akikamata nafasi ya 186 duniani. Anapatikana katika nafasi ya 79 katika viwango bora vipya vilivyotangazwa Jumatatu (Desemba 13).

Anasema mwaka huu umemwendea vyema licha ya changamoto zinazotokana janga la virusi vya corona.

“Umekuwa mwaka mzuri. Nilianza vyema kwa kushinda mashindano mawili Januari hapa nchini, ya mchezaji mmoja kwa mmoja na pia kufana ya wachezaji wawili kila upande. Hiyo ilinipa hamasa ya kutafuta mafanikio zaidi, hasa baada ya 2020 kuwa mwaka mgumu sana kwa wanamichezo. Mashindano mengi yaliahirishwa kwa sababu ya corona,” anasema.

Mwanafunzi huyo wa zamani wa shule ya msingi ya Mbagathi (Nairobi), King School (Burundi) , alizoa alama 200 kwa kushinda taji la Afrika (JB2 Sousse) nchini Tunisia mnamo Novemba 22 na kuruka kutoka 142 hadi nambari 93 duniani.

Anapolenga kutafuta ufanisi zaidi 2022 nje ya Afrika, anashukuru wazazi, familia, Shirikisho la Tenisi Kenya, ITF, kocha wake na Mungu kwa umbali huu amefika.

Okutoyi anakiri pia mwaka 2021 ulikuwa mgumu kwa sababu wakati mmoja katikati mwa mwaka usafiri ulitatizwa na vikwazo vya kudhibiti ugonjwa wa Covid-19.

“Hata hivyo, vilipolegezwa, niliweza kusafiri, kujiweka imara kiakili na kuwa tayari kimwili na kiakili kwa mashindano ambayo nilifaulu kushiriki nchini Misri, Afrika Kusini na Tunisia,” anaeleza.

Mwanafunzi huyo wa zamani wa shule ya msingi ya Mbagathi (Nairobi), King School (Burundi), alizoa alama 200 kwa kushinda taji la Afrika (JB2 Sousse) nchini Tunisia mnamo Novemba 22 na kuruka kutoka 142 hadi nambari 93 duniani.

Anapolenga kutafuta ufanisi zaidi 2022 nje ya Afrika, Okutoyi anashukuru wazazi wake, familia, Shirikisho la Tenisi Kenya, ITF, kocha wake na Mungu kwa umbali amefika.

You can share this post!

Visa vya corona Mwamba RFC vyasababisha mechi yake na KCB...

COVID-19: Vinara wa EPL wahimiza wachezaji kuchanjwa

T L