• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 9:50 AM
Man-United wafungulia mirefeji ya fedha na kumsajili beki Lisandro Martinez kutoka Ajax

Man-United wafungulia mirefeji ya fedha na kumsajili beki Lisandro Martinez kutoka Ajax

Na MASHIRIKA

BEKI Lisandro Martinez, 24, anatarajiwa kupiga jeki safu ya nyuma ya Manchester United baada ya kuagana na Ajax ya Ligi Kuu Uholanzi (Eredivisie) na kutua ugani Old Trafford kwa ada ya awali ya Sh6.9 bilioni ambayo itaongezeka hadi Sh8 bilioni.

Beki huyo aliyekuwa pia akiwaniwa na Arsenal, sasa anatazamiwa kuvalia jezi za Man-United kwa kipindi cha miaka mitano ijayo huku akitia mfukoni mshahara wa Sh17 milioni kwa wiki. Ujira huo ni sawa na ule ambao Victor Lindelof na Fred Paula Santos wanadumishwa nao ugani Old Trafford.

Kwa mujibu wa maelewano, Man-United ambao ni mabingwa mara 20 wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL), watakuwa huru kurefusha kandarasi ya Martinez kwa miezi 12 zaidi kutegemea matokeo yake.

Martinez anajivunia kusakatia Ajax mara 120 tangu abanduke rasmi kambini mwa Defensa y Justica ya Argentina kwa Sh888 milioni mnamo 2019. Amewahi pia kuchezea Newell’s Old Boys ya Argentina baada ya kupokea malezi ya kusakata soka kambini mwa Club Urquiza (2002-06) na Club Libertad (2006-2014).

Sogora huyo amechezea Argentina mara saba tangu mabingwa hao mara mbili wa Kombe la Dunia (1986, 1978) wamwajibishe kwa mara ya kwanza mnamo Machi 2019.

Anakuwa mchezaji wa tatu kuingia katika sajili rasmi ya Man-United muhula huu baada ya beki Tyrell Malacia aliyetokea Feyenoord ya Uholanzi kwa Sh2.2 bilioni na kiungo Christian Eriksen Christian Eriksen aliyetua Old Trafford bila ada yoyote.

Martinez ambaye mkataba wake na Ajax ulikuwa utamatike Juni 2025, anaungana na kocha mpya wa Man-United, Erik ten Hag, aliyewahi kumnoa kambini mwa Ajax kuanzia 2019.

Chini ya Hen Tag, Martinez alisaidia Ajax kunyanyua taji la Eredivisie mnamo 2021 na 2021 huku akizolea miamba hao ufalme wa Dutch Cup mnamo 2021. Ukubwa na upekee wa mchango wake ulimfanya kutawazwa Mchezaji Bora wa Mwaka kambini mwa Ajax mnamo 2021-22.

Ten Hag anayezidi kukisuka upya kikosi chake cha Man-United, anahemea sasa maarifa ya kiungo wa zamani wa Ajax, Frenkie de Jong, kutoka Barcelona ya Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga).

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

LISHE: Matunda ya pitahaya/ matunda ya joka

MAPISHI KIKWETU: Jinsi ya kuandaa supu ya asparagus

T L