• Nairobi
  • Last Updated December 5th, 2023 10:25 PM
Manchester United kukosa huduma za fowadi Rashford kwa miezi mitatu – Ripoti

Manchester United kukosa huduma za fowadi Rashford kwa miezi mitatu – Ripoti

Na MASHIRIKA

HUENDA fowadi matata wa Manchester United, Marcus Rashford akabakia nje ya uwanja kwa miezi mitatu baada ya kuamua kufanyiwa upasuaji wa bega mara tu kampeni za Euro 2020 zilipokamilika.

Kulingana na ripoti za Daily Telegraph na BBC, alifanyiwa vipimo kuhusiana na suala hilo, ambalo limemwandama tangu kukamilika kwa michuano ya Euro.

Hata hivyo, atalazimika kusubiri hadi mwisho wa Julai ili kupata mtaalam wa kumfanyia upasuaji huo.

Rashford alishiriki michuano mitano ya Euro 2020 kwa ajili ya taifa lake la Uingereza. Alikuwa miongoni mwa waliokabidhi Italia ushindi kwenye fainali baada ya kupoteza penalti.

Alikabili ubaguzi wa rangi baada ya michuano hiyo, watu walipoanika maneno ya kibaguzi mitandaoni, licha yake kumshajiisha Waziri Mkuu nchini humo kutoa lishe kwa wanfunzi wakati wa virusi vya corona.

Manchester United watajipima nguvu mnamo Jumapili dhidi ya Derby ugenini, wakijiandaa kwa ajili ya msimu ujao watakaoanza nyumbani dhidi ya Leeds United Agosti 14.

TAFSIRI NA: NDUNGI MAINGI

You can share this post!

Virgil van Djik tayari kurejea uwanjani – Jurgen Klopp

Mashindano ya Cecafa ya kina dada yaahirishwa hadi Agosti,...