• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 12:48 PM
Mbappe aongoza PSG kupepeta Strasbourg na kufungua pengo la alama nane kileleni mwa jedwali la Ligue 1

Mbappe aongoza PSG kupepeta Strasbourg na kufungua pengo la alama nane kileleni mwa jedwali la Ligue 1

Na MASHIRIKA

KYLIAN Mbappe aliongoza Paris Saint-Germain (PSG) kusajili ushindi wa 2-1 dhidi ya Strasbourg katika Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) mnamo Jumatano usiku.

Mechi hiyo ilikuwa ya kwanza kwa Mbappe kusakata tangu awe sehemu ya kikosi kilichowakilisha Ufaransa kwenye fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Argentina nchini Qatar mnamo Disemba 18, 2022.

Marquinhos aliwafungulia PSG ukurasa wa mabao katika dakika ya 14 kabla ya kujifunga na kusawazisha mambo mwanzoni mwa kipindi cha pili. PSG walikamilisha mchuano huo na wachezaji 10 pekee uwanjani baada ya fowadi Neymar Jr kuonyeshwa kadi nyekundu katika dakika ya 62.

Mbappe aliokoa jahazi ya PSG alipofunga mkwaju wa penalti sekunde chache kabla ya kipenga cha kuashiria mwisho wa mchezo kupulizwa. Penalti hiyo ilitokana na tukio la Mbappe kuchezewa visivyo na Gerzino Nyamsi ndani ya kijisanduku.

Ushindi huo ulidumisha PSG kileleni mwa jedwali la Ligue 1 kwa alama 44, nane zaidi kuliko nambari mbili Lens. Strasbourg kwa upande wao wanakamata nafasi ya 19 kwa pointi 11, tatu mbele ya Angers wanaovuta mkia.

MATOKEO YA LIGUE 1 (Jumatano):

PSG 2-1 Strasbourg

Ajaccio 1-0 Angers

Troyes 0-0 Nantes

Auxerre 2-3 Monaco

Clermont 0-2 Lille

Crest 2-4 Lyon

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Mshukiwa mmoja wa uhalifu auawa katika mtaa wa Mukuru...

Haaland aweka rekodi mpya ya ufungaji mabao EPL

T L