• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 11:53 AM
Haaland aweka rekodi mpya ya ufungaji mabao EPL

Haaland aweka rekodi mpya ya ufungaji mabao EPL

Na MASHIRIKA

ERLING Haaland aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kuwahi kufunga mabao 20 katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) haraka zaidi baada ya kuongoza waajiri wake Manchester City kupepeta Leeds United 3-1 mnamo Jumatano usiku ugani Elland Road.

Ushindi huo uliwawezesha Man-City ambao ni mabingwa watetezi wa EPL kupunguza pengo la alama kati yao na viongozi Arsenal hadi tano. Kufikia sasa, Man-City ya kocha Pep Guardiola inakamata nafasi ya pili jedwalini kwa pointi 35.

Baada ya makombora yake kadhaa kupanguliwa na kudhibitiwa na kipa wa Leeds, Haaland alipachika wavuni mabao mawili katika kipindi cha pili na kufikisha magoli 20 ligini kutokana na mechi 14 pekee.

Mabao yote mawili yaliyojazwa kimiani na Haaland yalichangiwa na Jack Grealish aliyepoteza nafasi nyingi za wazi. Bao jingine la Man-City lilifungwa na Rodri Hernandez huku Leeds wakifutiwa machozi na Pascal Struijk.

Nafuu zaidi kwa Man-City ni kwamba wana mechi moja zaidi ya akiba kuliko Newcastle United wanaowafuata kwa alama 33 jedwalini baada ya kutandaza jumla ya michuano 16.

Kichapo kutoka kwa Man-City kiliacha Leeds katika nafasi ya 15 kwa alama 15, tatu pekee kuliko Southampton wanaovuta mkia.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Mbappe aongoza PSG kupepeta Strasbourg na kufungua pengo la...

Mtu afa kwa kugongwa na basi lililotumbukia mtoni

T L