• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 7:47 PM
Mkenya ashinda Fukuoka Marathon kwa mara ya kwanza tangu 2015

Mkenya ashinda Fukuoka Marathon kwa mara ya kwanza tangu 2015

Na GEOFFREY ANENE

MKIMBIAJI Michael Githae amekuwa Mkenya wa kwanza kushinda mbio za Fukuoka Marathon nchini Japan katika kipindi cha miaka sita Jumapili.

Githae, 27, amenyakua taji kwa saa 2:07:51 ambao ni muda wake mpya bora baada ya kufuta ule wa 2:08:17 aliotimka akimaliza Fukuoka Marathon katika nafasi ya nne mwaka 2020. Bingwa huyo wa Shizuoka Marathon mwaka 2017 amefuatwa kwa karibu na Kyohei Hosoya (2:08:16), Mkenya James Rungaru (2:08:25), Shohei Otsuka (2:08:33) na Ryu Takaku (2:08:38) katika nafasi tano za kwanza.

Daisuke Uekado (2:08:56), Kohei Futaoka (2:09:14), Masaya Taguchi (2:09:35), Toshiki Sadakata (2:10:31) na Takuma Kumagai (2:10:41) wamekamilisha mduara wa 10-bora. Bingwa wa Boston Marathon 2018 Yuki Kawauchi na mshindi wa Hong Kong Marathon 2013 Ser-Od Bat-Ochir ni baadhi ya majina makubwa yaliyobwagwa na Githae.

Wakenya wengine ambao wamewahi kushinda Fukuoka Marathon ni Jackson Kabiga (1998), Samuel Wanjiru (2007), Josephat Ndambiri (2011), Joseph Gitau (2012), Martin Mathathi (2013) na Patrick Makau (2014 na 2015).

You can share this post!

TAHARIRI: Chanjo kwa wingi itasaidia kukabiliana na corona...

Rais atoa ahadi ya kuwainua walemavu

T L