• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 12:48 PM
Mkenya Ondoro ashinda Houston Marathon kwa mara ya pili, azoa Sh4.3m

Mkenya Ondoro ashinda Houston Marathon kwa mara ya pili, azoa Sh4.3m

Na GEOFFREY ANENE

MKENYA Dominic Ondoro ndiye mshindi wa Houston Marathon nchini Amerika.

Ondoro alikata utepe katika mbio hizo za kilomita 42 kwa saa 2:10:36 na kujizolea Sh4.3 milioni.

Ondoro, ambaye sasa ana mataji mawili ya Houston Marathon baada ya kutawala mwaka 2017, alifuatiwa na Muethiopia Ayana Tsedat (2:10:37) na Muamerika Teshome Mekonen (2:11:05) waliotia mfukoni Sh2.0 milioni na Sh864,033 mtawalia.

Hitomi Niiya kutoka Japan alitawala kitengo cha kinadada kwa muda wake bora wa saa 2:19:24 akifuatiwa na Waethiopia Muliye Dekebo (2:25:35) na Sintayehu Lewetegn (2:26:33).

Mkenya Wesley aliridhika na nafasi ya pili katika kitengo cha kilomita 21, akiandikisha muda wake bora wa 1:00:35, katikati ya mshindi Leul Gebresilase kutoka Ethiopia (1:00:34) na nambari tatu Mmoroko Mohamed El-Aaraby (1:00:58). Muethiopia Hiwot Gebrekidan (1:06:28), Muamerika Emily Sisson (1:06:52) na Muingereza Jess Warner-Judd walikamata nafasi tatu za kwanza katika kilomita 21 upande wa kinadada. Nafasi tatu za kwanza katika nusu-marathon zilizawadiwa Sh1.2 milioni, Sh740,599 na Sh493,733 mtawalia.

  • Tags

You can share this post!

KIGODA CHA PWANI: Ziara ya Raila Mombasa kulinda ngome yake...

Spika wa Bunge la Kericho Patrick Mutai mashakani baada ya...

T L