• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 5:01 PM
Motisha Arsenal baada ya kiungo tegemeo Thomas Partey kupona jeraha

Motisha Arsenal baada ya kiungo tegemeo Thomas Partey kupona jeraha

Na MASHIRIKA

TIMU ya Arsenal imepigwa jeki na marejeo ya beki matata Thomas Partey ambaye anatarajiwa leo kuunga kikosi cha kwanza dhidi ya Benfica kwenye marudiano ya Europa League baada ya kupona jeraha.

Partey ambaye ni raia wa Ghana, amekosa mechi tatu zilizopita za Arsenal, tangu apate jeraha la paja katika mchuano uliowashuhudia waajiri wake wakipepetwa 1-0 na Aston Villa mnamo Februari 6 uwanjani Villa Park.

Nyota huyo alisajiliwa kwa Sh6.3 bilioni mwanzoni mwa msimu huu kutoka Atletico Madrid ya Uhispania. Kuwepo kwake katika mechi ya leo Alhamisi kunatarajiwa kuwapa Arsenal motisha zaidi ya kuzamisha chombo cha Benfica baada ya masogora hao wa kocha Mikel Arteta kulazimishiwa na Benfica sare ya 1-1 kwenye mkondo wa kwanza uliowakutanisha jijini Roma, Italia mnamo Februari 18, 2021.

Marudiano ya leo kati ya vikosi hivyo yataandaliwa jijini Athensm Ugiriki huku Arsenal wakijivunia bao la ugenini walilofungiwa na kiungo chipukizi Bukayo Saka katika mechi ya awali.

Arteta atatarajia wachezaji wake kusajili ushindi dhidi ya Benfica na kuweka hai matumaini ya kutia kapuni ubingwa wa Europa League msimu huu kwa kuwa ndiyo njia ya pekee kwa Arsenal kufuzu kwa soka ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) msimu ujao.

Partey, 27, amepangwa katika kikosi cha kwanza cha Arsenal mara tisa pekee kufikia sasa ligini huku akichezeshwa kwenye soka ya bara Ulaya mara moja pekee.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Serikali yaahidi kusaidia Kenya Morans kujiandaa kwa...

Sevilla wataka Man-United waweke mezani Sh9.5 ili...