• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 2:31 PM
Mrushaji sahani anayelenga kuwa kama mtupaji bora Sandra Perkovic

Mrushaji sahani anayelenga kuwa kama mtupaji bora Sandra Perkovic

NA PATRICK KILAVUKA

BAADA ya kujitosa kwa udi na uvumba katika mchezo wa kurusha sahani na kuwa bingwa wa shule katika mashindano baina ya vidato katika shule yake ya Wasichana ya Highridge,Westland mrushaji sahani Minneh Mboya, 17, anaazimia kugonga vichwa vya habari katika fani hii alivyo mrushaji wa kimataifa raia wa Croatia Sandra Perkovic ambaye amewahi kurusha umbali wa mita 71.41.

Alianza maandalizi ya mashindano ya michezo ya shule za upili na katika kaunti ndogo ya Westlands na katika ngarambe hiyo, japo alitawazwa malkia wa tatu bora katika urushaji wa sahani katika kaunti ndogo ya Westlands kwa kutupa umbali wa mita 44.72  nyuma ya Stella Nekesa wa sekondari ya Kabete Vetlab (mita 45.20) na Chesire Wachira wa Kianda School (mita 44.78).

Mrushaji huyu ni mwanafunzi wa Kidato cha Tatu katika shule ya upili ya wasichana ya Highridge, kaunti ndogo ya Westlands.

Alianza safari ya elimu katika Shule ya Msingi ya Daima, Nairobi.

Mrushaji sahani Minneh Mboya akiwa na wanariadha wengine ambao walishiriki katika mbio mbalimbali katika mashinadano ya riadha ya shule za upili za kaunti ndogo ya Westlands yaliyoandaliwa kwenye Shule ya Upili ya Nairobi. PICHA | PATRICK KILAVUKA

Alianza kurusha sahani baada ya kupata ushawishi kutoka kwa mrushaji mwingine shuleni anakosomea na kuzamia kwa kuwa na ari na kiu ya kupata ujuzu zaidi. Alianza kufanya mazoezi kwa bidii ya mchwa.

Anasema mwanzoni, alikuwa akirusha mita 16, japo analenga kuvurumisha sahani hadi mita 30 kuliko alirusha kwenye mashindano kujiboresha zaidi.

Mrushaji sahani Minneh Mboya aliyeibuka wa tatu bora katika mashindano ya riadha ya kaunti ndogo ya Westlands akionyesha anavyorusha sahani. PICHA | PATRICK KILAVUKA

Akiwa na mkinzani wake wa karibu Melissa Glory shuleni na ambaye wanajinoa naye kila mara kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa, Minneh ameimarisha mbinu anuwai za kurusha sahani huku akizingatia ufundishaji na uelekezi wa Okuku.

Ingawa huu ni mwaka wake kwanza kurusha sahani, anasema amejitwika jukumu la kuhakikisha weledi wake umeendelea kudhihirika hatua kwa hatua hadi ngazi za kikaunti, kimaeneo, kitaifa na kimataifa siku za usoni.

Ametuzwa vyeti vya kuwa bora shuleni.

Kuwa mrushaji wa haiba, anaeleza kwamba unafaa kuwa unakula lishe bora na linaloimarisha nishati mwili pamoja na kutia bidii ya mchwa katika kujinoa na kusikiza mawaidha ya mwelekezi.

Minneh anasema umbali ametua ni kwa sababu ya kukumbatiwa na wazazi, wanafunzi wenza, walimu na mwalimu mkuu ambao wamemtia moyo hali ambayo imempelekea kukabiliana na changamoto kama kukata tamaa na shauku ya kutofanya vyema na hatua kwa hatua, ameyaona matunda ya bidii yake na ukuzaji wa kipaji chake.

Matarajio yake sasa ni kutupa sahani viwango vya juu zaidi kwani anasema safari yake imeng’oa nanga.

  • Tags

You can share this post!

MAPISHI KIKWETU: Nyama, brokoli na wali

Mabaki ya wahanga 587 wa mauaji ya kimbari yafukuliwa...

T L