• Nairobi
 • Last Updated May 19th, 2024 6:50 AM
MAPISHI KIKWETU: Nyama, brokoli na wali

MAPISHI KIKWETU: Nyama, brokoli na wali

NA MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 10

Muda wa mapishi: Dakika 40

Walaji: 4

Vinavyohitajika

 • mafuta ya mzeituni
 • kilo 1 ya nyama ya ubavu iliyokatwa vipande vyembamba
 • punje 3 za vitunguu saumu, sagasaga
 • vitunguu maji 2, kata vipande vyembamba
 • vikombe 4 vya brokoli
 • vijiko 2 vya wanga
 • kikombe 1 cha maji
 • vijiko 2 sosi ya soya
 • vijiko 2 vya sukari
 • kijiko 1 cha tangawizi iliyokatwa
 • pilipili nyekundu
 • mchele kiasi kikombe 1 1/4
 • vikombe 3 vya mchuzi wa kuku
 • chumvi

Maelekezo

Ili kupika nyama ya ng’ombe na brokoli, pasha mafuta ya mizeituni kwenye sufuria juu ya moto wa kati.

Ongeza nyama iliyokatwa nyembamba na upike hadi iwe rangi ya hudhurungi, kama dakika 10.

Mara tu inapokuwa ya hudhurungi, toa kutoka kwenye sufuria na kuiweka kando.

Katika sufuria iyo hiyo, ongeza vitunguu maji vilivyokatakatwa, vitunguu saumu  na vitunguu vya kijani. Pika kwa dakika moja, huku ukichochea mara kwa mara.

Kisha, ongeza brokoli na upike kwa muda wa dakika tano hadi brokoli liwe laini zaidi.

Ili kutenegeneza mchuzi, katika bakuli changanya sosi ya soya, sukari, tangawizi iliyosagwa, na pilipili.

Ongeza wanga na maji na koroga hadi vichanganyike vizuri.

Ongeza mchuzi huu kwenye sufuria na upike hadi uanze kuwa mzito, kama dakika tano hivi. Rudisha nyama ya ng’ombe na koroga ili kuchanganya, halafu pika kwa dakika mbili au tatu za ziada. Kisha, weka kando ipoe kidogo kisha pakua na ufurahie.

 • Tags

You can share this post!

Oparesheni barabarani kupunguza visa vya ajali

Mrushaji sahani anayelenga kuwa kama mtupaji bora Sandra...

T L