• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 6:50 AM
Msimu mpya wa mbio za nyika kuanza Oktoba 14 mjini Machakos

Msimu mpya wa mbio za nyika kuanza Oktoba 14 mjini Machakos

Na GEOFFREY ANENE

MSIMU wa mbio za nyika wa 2023-2024 utaanza Oktoba 14, Shirikisho la Riadha nchini Kenya (AK) lilitangaza Jumatatu.

AK ilisema kuwa raundi ya kwanza ya mbio za nyika itaandaliwa katika bustani ya Machakos People’s Park katika Kaunti ya Machakos, wiki chache tu baada ya msimu wa riadha za uwanjani kukamilika mwezi Septemba.

Wanariadha kisha wataonyeshana kivumbi katika raundi ya pili katika eneo la Kapsokwony katika Mlima Elgon kaunti ya Bungoma mnamo Oktoba 21.

Baadhi ya nyota ambao wameshiriki mbio za nyika za Machakos hapo awali ni pamoja na bingwa mara mbili wa dunia mbio za mita 5,000 Hellen Obiri, malkia mpya wa mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na maji Winfred Yavi, ambaye alichukua uraia wa Bahrain, mshikilizi wa rekodi ya dunia mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na maji Beatrice Chepkoech na mshindi wa nishani ya fedha ya kilomita 21 duniani Daniel Simiu.

Beatrice Chebet aliyeshinda mataji ya dunia ya Mbio za Nyika nchini Australia na kilomita tano nchini Latvia mwaka 2023 alisema majuzi kuwa analenga kutetea taji lake la nyika jijini Belgrade nchini Serbia mnamo Machi 30, 2024.

  • Tags

You can share this post!

Leo ni siku ambayo Rais Ruto aliahidi kukutana na Museveni...

Afanyiwa kiini macho akapapasa nyani akidhani ni kimada wake

T L