• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 12:48 PM
Ndondi: Okoth ajikwaa mashindano ya Madola nchini Uingereza

Ndondi: Okoth ajikwaa mashindano ya Madola nchini Uingereza

NA CHARLES ONGADI

KENYA ilianza vibaya mashindano ya ndondi ya Jumuia ya Madola nahodha Nick ‘Commander’ Okoth aliposhindwa na Keevin Allicock wa Guyana, Jumamosi.

Katika pigano hilo, Okoth alijaribu kutumia kila mbinu kuzoa alama katika raundi zote tatu ila mpinzani wake alionekana kumzidi maarifa.

Majaji wote watano katika pigano hilo la uzito wa unyoya walimpatia Keevin Allicock ushindi sawa wa alama 30-27 hivyo kupiga breki juhudi za Okoth kusonga mbele katika mashindano hayo.

Okoth ambaye ni mshindi wa medali ya shaba katika mashindano ya Madola yaliyoandaliwa Delhi nchini India mwaka wa 2010 kwa mara nyingine atarudi nyumbani mikono mitupu.

Katika Michezo ya Olimpiki ya Tokyo, nchini Japan, Okoth alikuwa miongoni mwa mabondia wanne nchini waliobanduliwa katika hatua ya mchujo.

Aidha, matokeo haya yanaiwacha Kenya na mabondia watatu, Christine Ongare (Minimum), Shaffi Bakari( bantam) na Elizabeth Andiego (Middle).

Shaffi Bakari anatarajiwa kupanda ulingoni siku ya Jumanne kukabiliana na Rukmal Prsasanna wa Sri Lanka katik apigano ambalo mshindi atakutana na Mensah Abraham wa Ghana .

Kisha siku ya Jumatano, itakuwa ni zamu ya mabondia wawili wa kike Christine ongare na Elizabeth Ongare ambao wako katika hatua ya robo fainali baada ya kupata ushindi wa chee katika hatua ya muondoano.

Ongare ambaye ni mshindi wa medali ya shaba katika Michezo ya Madola mwaka wa 2018 yaliyoandaliwa Gold Coast nchini Australia, atakabiliana na Dhillon Prinyanka wa Canada.

Andiego naye atakabiliana na Parker C wa Australia katika pigano ambalo mshindi anafuzu nusu fainali na kujiweka katika nafasi nzuri ya kuvvuna medali.

  • Tags

You can share this post!

Uhuru aelezea manufaa ya Nairobi Expressway

Liverpool walipua Man-City katika gozi la Community Shield

T L