• Nairobi
  • Last Updated May 12th, 2024 5:17 PM
Nyota wa kigeni wa Olimpiki waingia Kip Keino Classic

Nyota wa kigeni wa Olimpiki waingia Kip Keino Classic

Na AYUMBA AYODI

ZIKISALIA zaidi ya wiki mbili mashindano ya Kip Keino Classic yaandaliwe jijini Nairobi hapo Septemba 18, mabingwa wa Olimpiki Wojciech Nowicki na Peruth Chemutai ni miongoni mwa wanariadha waliothibitisha kushiriki makala hayo ya pili.

Mkurugenzi wa mashindano Barnaba Korir alifichua Septemba 1 kuwa Kip Keino Classic inavutia washiriki wengi waliokuwa Olimpiki 2020 zilizofanyika nchini Japan mnamo Julai 23 hadi Agosti 8.

Raia wa Poland, Nowicki alitwaa ubingwa wa fani ya uwanjani ya Hammer Throw baada ya kuandikisha mtupo wa mita 82.52 naye Mganda Chemutai aliduwaza wengi akibeba taji la mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na maji kwa rekodi ya kitaifa ya dakika 9:01.45 jijini Tokyo.

Chemutai alifuatiwa kwa karibu na Mwamerika Courtney Frerichs (9:04.79) huku Mkenya na mshindi wa medali ya fedha ya Olimpiki 2016 Hyvin Jepkemoi aliyepigiwa upatu, akiridhika na nishani ya shaba (9:05.39).

“Ni kitu cha kujivunia kama taifa kupata wanariadha watajika wakitangaza kuwa watakuja Kenya kwa mashindano hayo,” alisema Korir.

Aliongeza kuwa wenyeji Kenya watajitahidi kuandaa mashindano ya kufana ugani Kasarani.

“Jinsi mambo yalivyokuwa katika siku tano za Riadha za Dunia za Under-20 majuzi zilizofaulu, tunaahidi kuwa na mashindano mazuri ya siku moja ugani Kasarani,” alieleza Korir.

Alifichua kuwa Shirikisho la Riadha Kenya (AK) linazungumza na serikali kuruhusu mashabiki 20,000 uwanjani humo.

Serikali haikuruhusu mashabiki wakati wa makala ya kwanza pamoja na Riadha za Dunia za Under-20.

TAFSIRI: GEOFFREY ANENE

  • Tags

You can share this post!

Kitany na DCI wapinga kinga ya Linturi kortini

Barcelona wamsajili De Jong, Griezmann arejea Atletico