• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 6:40 PM
Obiri ang’ara mbio za mita 10,000

Obiri ang’ara mbio za mita 10,000

Na GEOFFREY ANENE

BINGWA wa dunia wa mbio za mita 5,000 Hellen Obiri alitwaa ubingwa wa mbio za mita 10,000 ugani Kasarani, Jumamosi.

Mshindi huyo medali ya fedha ya Olimpiki ya mbio za mita 5,000 alikuwa ameapa kutumia tuzo ya kifahari ya Wanawake ya Forbes aliyopata mapema juma hili kama kichocheo cha kushinda mbio hizo za kuzunguka uwanja mara 25. Alitimiza ahadi hiyo kwa kukamilisha umbali huo kwa dakika 31:24.7, sekunde 4.53 mbele ya mpinzani wake wa karibu Eva Cherono (31:29.6) naye Vicoty Chepng’eno akaridhika katika nafasi ya tatu (31:42.9).

Naye Mark Otieno alidhihirisha tena nani mbabe katika mbio za mita 100 kati yake na Ferdinand Omanyala alipombwaga katika fainali. Otieno, ambaye alimlemea Omanyala katika nusu-fainali Ijumaa, alimuonyesha kivumbi tena alitawala fainali kwa sekunde 10.24. Omanyala aliridhika tena na nafasi ya pili kwa sekunde 10.40 naye Tazana Kamanga akamaliza akawa wa tatu (10.49).

Duru ijayo itafanyika Aprili 2-3.

Matokeo (Machi 13):

Mita 1,500 (wanawake)

Josephine Chelagat dakika 4:10.6

Winny Chebet 4:11.0

Loice Chemnung 4:15.2

Joyce Munani 4:17.2

Vivian Kosgei 4:17.6

Juliet Cherubet 4:18.9

Monica Margaret 4:23.1

Matembezi ya kilomita 15 (wanaume)

Samuel Gathimba saa 1:01:54

Simon Wachira 1:06:25

Dominic Ndigiti 1:07:56

Erick Shikuku 1:08:28

Mita 400 (wanaume)

Stanley Kieti sekunde 46.9

Cleophas Kipruto 47.15

Joseph Poghisio 47.28

Geoffrey Kapelo 47.34

Gabriel Larmoi 47.41

Vincent Kosgei 47.57

Jeremiah Mutai 47.73

Mita 400 (wanawake)

Evangeline Makena sekunde 54.10

Joan Cherono 54.32

Veronica Mutua 54.57

Gladys Musyoki 55.55

Sylvia Chesebe 55.91

Mita 100 (wanaume)

Mark Otieno 10.24

Ferdinand Omanyala 10.40

Tazana Kamanga 10.49

Tarsis Orogot 10.75

Peter Mwai 10.78

Elijah Mathew 10.79

Samuel Imeta 10.91

Mita 100 (wanawake)

Maximila Imali sekunde 11.95

Doreen Waka 12.19

Monica Safania 12:41

Susan Nyambura 12:55

Emily Gesare 13.15

Mita 10,000 (Wanawake)

Hellen Obiri dakika 31:24.7

Eva Cherono 31:29.6 (muda wake bora)

Vicoty Chepng’eno 31:42.9

Brillian Jepkorir 32:05.2

Irene Kimais 32:32.10

Naum Chepng’eno 32:42.5

Agnes Mumbua 33:06.7

Beatrice Cherubet 33:25.3

You can share this post!

Aguero akomesha ukame wa miezi 14 wa mabao ya EPL katika...

Yaya aliyewajeruhi watoto wa mwajiri aliyemfuta kazi atiwa...