• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 3:09 PM
Aguero akomesha ukame wa miezi 14 wa mabao ya EPL katika gozi kati ya Man-City na Fulham

Aguero akomesha ukame wa miezi 14 wa mabao ya EPL katika gozi kati ya Man-City na Fulham

Na MASHIRIKA

SERGIO Aguero alifunga bao lake la kwanza tangu Januari 2020 mnamo Jumamosi usiku na kusaidia waajiri wake Manchester City kusajili ushindi wa 3-0 dhidi ya Fulham uwanjani Craven Cottage.

Ni ushindi uliowezesha masogora hao wa kocha Jurgen Klopp kufungua pengo la alama 17 kileleni mwa jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) japo nambari mbili Manchester United ambao wana pointi 54 wangali na mechi mbili zaidi za kusakata ili kufikia idadi ya michuano ambayo imepigwa na Man-City.

Huku ushindi wa Man-City ukiwafanya sasa kunusia taji la EPL, matumaini ya Fulham kusalia kwenye kampeni za kipute hicho msimu ujao yanazidi kudidimia.

Kikosi hicho kwa sasa kinashikilia nafasi ya 18 kwa alama 26 na kikosi katika mduara hatari wa kushushwa ngazi kwa pamoja na West Bromwich Albion na Sheffield United ambao wamejizolea alama 18 na 14 mtawalia.

Baada ya kipindi cha kwanza kukamilika kwa sare tasa, Man-City walianza kampeni za kipindi cha pili kwa matao ya juu na wakafunguliwa ukurasa wa mabao na beki John Stones aliyekamilisha krosi ya Joao Cancelo katika dakika ya 47.

Goli la pili la Man-City wanaotiwa makali na kocha Pep Guardiola, lilifumwa wavuni na Gabriel Jesus kunako dakika ya 56, kabla ya Aguero kufunga penalti dakika nne baadaye. Penalti hiyo ilichangiwa na tukio la Tosin Adarabioyo kumchezea vibaya kiungo Ferran Torres.

Man-City wangalifunga mabao zaidi katika kipindi cha pili ila mafowadi wao wakashindwa kumzidi ujanja kipa Alphonse Areola aliyesalia imara katikati ya michuma.

Guardiola aliteua kuwajibisha mabeki watatu pekee huku Jesus na Aguero wakipangwa pamoja katika safu ya mbele kwa mara ya kwanza tangu Februari 2020. Wanasoka Raheem Sterling, Kevin de Bruyne na Ilkay Gundogan waliwajibishwa katika safu ya kati.

Fulham kwa sasa watakuwa wenyeji wa Leeds United ugani Craven Cottage kwa ajili ya mchuano wao ujao ligini mnamo Machi 19, 2021.

Kwa upande wao, Man-City wamepangwa kurudiana na Borussia Monchengladbach ya Ujerumani katika mechi ya hatua ya 16-bora ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) uwanjani Puskas Arena jijini Budapest, Hungary mnamo Machi 16. Baada ya hapo, wataelekea ugani Goodison Park kuchuana na Everton kwenye robo-fainali za Kombe la FA mnamo Machi 20, 2021.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Quins, Blak Blad hatimaye wazoa ushindi Ligi Kuu ya Raga

Obiri ang’ara mbio za mita 10,000