• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 6:40 PM
Obiri kivutio mbio za nyika nchini Northern Ireland

Obiri kivutio mbio za nyika nchini Northern Ireland

Na GEOFFREY ANENE

MALKIA wa mbio za mita 5,000 na mbio za nyika, Hellen Obiri atatimka mbio za nyika za kimataifa za Northern Ireland uwanjani Billy Neill Country Park jijini Belfast mnamo Januari 22.

Kwa sasabu hiyo Obiri, 32, ambaye ni bingwa wa Kenya, Afrika, Jumuiya ya Madola na dunia wa mbio za mita 5,000, atakosa katika mbio za nyika za kitaifa zitakazofanyika siku hiyo uwanjani Lobo mjini Eldoret. Mwanajeshi huyo alishinda taji la dunia la mbio za nyika mjini Aarhus, Denmark mwaka 2019.

Ameelekea Belfast baada ya kutwaa taji lake la tano kwenye mbio za nyika za majeshi (KDF) uwanjani Moi Air Base jijini Nairobi mnamo Januari 7. Alishiriki mbio hizo wiki moja baada ya ugonjwa wa Covid-19 kumnyima fursa ya kutimka kwenye mbio za San Silvestre Vallecana jijini Madrid mnamo Desemba 31, 2021.

Kukosekana kwake katika mbio za nyika wikendi hii kunamaanisha kuwa KDF itawategemea Sheila Chepkirui, Pauline Korikwang, Perine Nengapi, Valentine Chepkoech na Joyce Chepkemoi kutafuta ushindi. Zaidi ya wakimbiaji 500 kutoka timu mbalimbali zikiwemo Police na Prisons watakuwa uwanjani Lobo mnamo Jumamosi.

Baadhi ya wakimbiaji ambao Obiri atakabiliana nao mjini Belfast ni Kate Avery, Eleanor Bolton, Abbie Donnelly na Jess Gibbon.

You can share this post!

Vihiga Queens, Malkia Strikers kuwania tuzo ya wanamichezo...

Mameneja 9 wa Kenya Power kortini kuhusiana na stima kupotea

T L