• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 1:02 PM
Vihiga Queens, Malkia Strikers kuwania tuzo ya wanamichezo ya SOYA

Vihiga Queens, Malkia Strikers kuwania tuzo ya wanamichezo ya SOYA

Na GEOFFREY ANENE

WENYEJI wa tuzo za kufahari za wanamichezo bora wa Kenya, SOYA wametangaza wawaniaji wa mwaka wa kitengo cha timu za kinadada.

Orodha hiyo ya timu tano inajumuisha Kenya Lioness. Hawa ni mabingwa wa mpira wa vikapu wa Zoni ya Tano. Vipusa wa kocha George Mayienga walianza kampeni kwa kulimwa na wenyeji Rwanda 77-45, wakazaba Sudan Kusini 66-48 na kuachilia uongozi wa alama 25 wakazimwa na Misri 107-106 katika mechi za makundi.

Kisha, walichabanga Rwanda 79-52 katika nusu-fainali kabla ya kuduwaza Misri 99-83 katika fainali na kuingia Kombe la Afrika (AfroBasket). Walishinda Cape Verde pekee katika AfroBasket wakimaliza nambari tisa kati ya washiriki 12 jijini Yaounde, Cameroon.

Timu ya raga ilitwaa Kombe la Safari Sevens na kuridhisha katika mashindano ya kualikwa ya Madrid na Tunisia pia Olimpiki 2020 nao Vihiga Queens walitawala mashindano Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) jijini Nairobi. Vihiga ilifuzu kushiriki Klabu Bingwa Afrika nchini Misri ilikopiga AS FAR ya Morocco na kupoteza dhidi ya Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini) na Rivers Angeles (Nigeria). Timu ya voliboli ya ufukweni ilinyakua ubingwa wa Afrika nchini Morocco ikiingia Olimpiki. Malkia Strikers pia ilivuna tiketi ya Olimpiki baada ya kuchapa Misri, Botswana, Cameroon na Nigeria ikirejea Olimpiki tangu 2004.

  • Tags

You can share this post!

‘Hasla’ anatetemeshwa na umaarufu wangu –...

Obiri kivutio mbio za nyika nchini Northern Ireland

T L