• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 6:40 PM
Olunga aibuka Mfungaji Bora dimba la Asia kwa mabao 9

Olunga aibuka Mfungaji Bora dimba la Asia kwa mabao 9

Na GEOFFREY ANENE

Nahodha wa Harambee Stars, Michael Olunga aliibuka mfungaji bora wa Klabu Bingwa Asia 2021 baada ya dimba hilo kutamatika Novemba 23.

Mshambuliaji huyo wa kati wa Al Duhail nchini Qatar alitikisa nyavu mara tisa katika mashindano hayo ya timu 40 yaliyoandaliwa kati ya Aprili 14 na Novemba 23. Mabao yake yote yalipatikana katika mechi za Kundi C (Ukanda wa Magharibi) dhidi ya Al Shorta kutoka Iraq (mawili), Esteghlal kutoka Iran (matano) na Al Ahli Saudi (mawili) mjini Jeddah, Saudi Arabia.

Al Duhail ilikamilisha kundi lake katika nafasi ya pili nyuma ya Esteghlal, kwa hivyo haikusonga mbele. Ilizoa ya tuzo ya Sh14.5 milioni kwa kila ushindi na Sh1.1 milioni kwa kila sare). Al Duhail pia inaaminika kutia kapuni ruzuku ya Sh5.0 milioni kwa kila mchuano iliosakata.

Olunga ni mchezaji wa kwanza kutoka Al Duhail kuibuka mfungaji bora tangu dimba hilo lianzishwe.Katika kampeni yake ya kwanza kabisa, Olunga alimaliza mbele ya wachezaji wa Jeonbuk Hyundai Motors Gustavo na Modou Barrow waliopachika mabao manane na sita, mtawalia.

Al Hilal ilinyakua ubingwa wa Klabu Bingwa Asia 2021 kwa kulima Pohang Steelers kutoka Korea Kusini 2-0 katika fainali Jumanne. Al Duhail pia itashiriki Klabu Bingwa Asia msimu ujao baada ya kujikatia tiketi kwa kuwa nambari mbili kwenye Ligi Kuu ya Qatar msimu 2020-2021 nyuma ya Al Sadd

You can share this post!

Lempurkel aomba aachiliwe kwa dhamana kabla ya kesi...

Wasimamizi wapya wa Ligi Kuu kuteuliwa leo

T L