• Nairobi
  • Last Updated May 12th, 2024 5:17 PM
Pigo Pogba akijiondoa katika kikosi kwa jeraha

Pigo Pogba akijiondoa katika kikosi kwa jeraha

Na MASHIRIKA

KIUNGO Paul Pogba ameondolewa katika kikosi cha timu ya Ufaransa kinachojiandaa kwa mchujo wa kufuzu kwa Kombe la Dunia.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 aliumia pajani Jumatatu wakati wa mazoezi ambapo ripoti ya daktari imesema hawezi kucheza Jumamosi dhidi ya Kazakhstan nyumbani na pia ugenini dhidi ya Finland, mwezi ujao.

Ufaransa wanahitaji ushindi katika mechi hizo mbili ili wafuzu kwa fainali hizo zitakazofanyika Qatar mwakani. Kukosekana kwake, kadhalika kutamkosesha usingizi kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer ambaye tayari atapanga kikosi chake bila nyota kadhaa wanaouguza majeraha.

Tayari staa huyo atakosa kucheza dhidi ya Watford mwezi ujao kwenye ligi kuu ya Premia (EPL) kutokana na marufuku ya mechi tatu.Pogba alipigwa marufuku hiyo alipoonyeshwa kadi na kutolewa uwanjani katika mechi yao dhidi ya Liverpool mnamo Oktoba 24 ambayo walicharazwa 5-0.

Wachezaji wengine wa Manchester United watakaozikosa mechi kadhaa kutokana na majeraha ni pamoja na Mfaransa Raphael Varane, beki wa kushoto Luke Shaw na mshambuliaji Edinson Cavani.

Rashford ameondolewa katika kikosi cha Uingereza kutokana na jeraha na sasa hatacheza mechi za kufuzu dhidi ya Albania na San Marino. Straika huyo mwenye umri wa miaka 24 hajachezea Uingereza tangu wakati wa mechi za Euro 2020, na sasa nafasi yake kikosini imechukuliwa na Emile Smith Rowe wa Arsenal.

Kukosekana kwa nyota hao kutamuongezea presha kocha Solskajaer ambaye amekuwa akipokea foka za kila aina kutoka kwa mashabiki.

You can share this post!

Washukiwa wawili wakamatwa kwa kuiba paipu za maji

Muuguzi asakwa kwa dai la kunajisi mwanafunzi

T L