• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 10:08 PM
Red Star Belgrade anayochezea Mkenya Richard Odada kualika AC Milan bila mashabiki

Red Star Belgrade anayochezea Mkenya Richard Odada kualika AC Milan bila mashabiki

Na GEOFFREY ANENE

MABINGWA wa Serbia, Red Star Belgrade, ambao wameajiri chipukizi Mkenya Richard Odada wameshindwa katika juhudi zao za kutaka mechi yao ya Ligi ya Uropa dhidi ya AC Milan ihudhuriwe na mashabiki.

Kupitia mitandao yake ya kijamii, Red Star imethibitisha Jumanne kuwa iliomba serikali iruhusu mashabiki na kuihakikishia kuwa watatii masharti yote ya afya ya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

“Hata hivyo, maafisa kutoka serikali wanaohusika na kukabiliana na majanga walisema kuwa hawawezi kulegezea kamba yeyote. Kwa hivyo, hakuna mashabiki watakubaliwa uwanjani tutakapoalika Milan kwenye Ligi ya Uropa. Hawaruhusiwi kuhudhuria mashindano mengine yoyote nchini Serbia,” ilisema klabu hiyo ambayo itaalika miamba hao wa Italia jijini Belgrade kwa mechi ya raundi ya 32-bora hapo Februari 18. Zitarudiana jijini Milan mnamo Februari 25.

Red Star ilikung’uta wenyeji Novi Pazar katika mechi ya kwanza ligini mwaka 2021 hapo Februari 7 ambayo kiungo Odada alitarajiwa kushiriki, lakini hakuwa kikosini. Mkenya huyo, ambaye tetesi zinasema anatafuta uraia wa Serbia baada ya kuishi nchini humo tangu 2017, alisaini kandarasi yake ya kwanza ya malipo na Red Star mnamo Januari 1, 2021.

  • Tags

You can share this post!

Omanga na wenzake wapata afueni

Mshukiwa wa ulaghai wa mamilioni azuiwa kusafiri