• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 5:50 AM
Shirikisho kuandaa vipute vingi kunoa Wapwani katika magongo

Shirikisho kuandaa vipute vingi kunoa Wapwani katika magongo

NA ABDULRAHMAN SHERIFF

MWENYEKITI wa Chama cha mpira wa magongo Kaunti ya Mombasa (MCHA), Oliver Mascarenhas amesema chama chake kitajitahidi kuandaa mashindano mara kwa mara ili vijana wapate kujiendeleza na kuinua vipaji vyao.

Akiongea mwishoni mwa mashindano ya MCHA Hockey 5’s Festival yaliyoandaliwa katika Serani Sports, Mascarenhas alisema ana imani kubwa ya wadhamini kujitokeza.

“Tuna imani kubwa kama tutakuwa na mashindano mengi, vijana wetu wataweza kunoa vipaji vya uchezaji wao na kuwa na nafasi nzuri ya kuvutia wateuzi wa timu za taifa,” akasema Mascarenhas.

Kinara huyo alizisifu timu zote zilizoshiriki kwa kucheza mchezo wa hali ya juu huku wachezaji wakidumisha nidhamu ya hali ya juu.

Katika mashindano hayo ambayo yalivutia timu 14, Kenya Police ‘B’ kutoka Nairobi waliibuka washindi baada ya kuwalaza ndugu zao wa Kenya Police ‘A’ 2-0 kupitia kwa mikwaju ya penalti.

Mechi ilimalizika timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1.

  • Tags

You can share this post!

KAULI YA WALLAH BIN WALLAH: Ukitumia ubongo wako vizuri...

Nabirye ateuliwa kikosi cha Uganda michuano ya AWCON

T L