• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 12:18 PM
Shujaa, Lionesses waanza kujinoa tena baada ya kupumzika wiki moja

Shujaa, Lionesses waanza kujinoa tena baada ya kupumzika wiki moja

Na GEOFFREY ANENE

TIMU ya taifa ya raga ya wachezaji saba kila upande ya wanaume almaarufu Shujaa imerejelea mazoezi Machi 8 baada ya kupumzika juma moja.

Vijana wa kocha Innocent “Namcos” Simiyu walirejea nchini mapema wiki iliyopita kutoka Uhispania walikokamilisha mashindano mawili ya Madrid Sevens katika nafasi ya pili mnamo Februari 20-21 na Februari 27-28.

“Tulipimwa virusi vya corona Ijumaa asubuhi (Machi 5) na kila mtu yuko sawa,” alieleza Simiyu hapo Jumapili.

Waliowakilisha Kenya nchini Uhispania dhidi ya Argentina, Amerika, Ureno, Uhispania na Chile ni Nelson Oyoo na Herman Humwa (manahodha), Alvin Otieno, Bush Mwale, Harold Anduvati, Vincent Onyala, William Ambaka, Daniel Taabu, Johnstone Olindi, Mark Kwemoi, Tony Omondi, Billy Odhiambo, Derrick Keyoga, Jacob Ojee, Jeff Oluoch na Alvin Marube. Wachezaji wengine wa Shujaa ambao hawakusafiri akiwemo nahodha wa zamani Andrew Amonde, waliendelea na mazoezi kama kawaida uwanjani RFUEA.

Pamoja na timu ya kinadada ya Kenya Lionesses, ambayo ilikamilisha Madrid Sevens katika nafasi ya mwisho mnamo Februari 20-21 na nambari mbili Februari 27-28, wanatarajiwa kuingia kambi ya Olimpiki hivi karibuni.

Shujaa na Lionesses zilifuzu kushiriki Olimpiki mwaka 2019 wakati zilikamilisha Kombe la Afrika katika nafasi ya kwanza na nambari mbili nchini Afrika Kusini na Tunisia, mtawalia.

Zinatarajiwa kuelekea mjini Dubai katika Milki za Kiarabu kwa mashindano mengine mawili baadaye mwezi huu wa Machi.

  • Tags

You can share this post!

Wananyuki wawika baada ya kuwanyuka wapinzani wao wa jadi...

Chelsea wakomoa Everton na kuweka hai matumaini ya kumaliza...