• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 10:50 AM
Tennis Kenya kuadhimisha miaka 100 kwa kuombea Okutoyi mafanikio mema na kupanda miti Kasarani

Tennis Kenya kuadhimisha miaka 100 kwa kuombea Okutoyi mafanikio mema na kupanda miti Kasarani

Na GEOFFREY ANENE

SHIRIKISHO la Tenisi Kenya (Tennis Kenya) litapanda miti 100 katika sehemu ya shamba la Kasarani ambalo serikali imelitengea kujenga viwanja 24 hapo Desemba 20.

Tennis Kenya imesema Jumanne kuwa itaandaa sherehe siku hiyo za kuadhimisha miaka 100 tangu lianzishwe. Mwanatenisi nyota Angella Okutoyi pia ataombewa katika sherehe hizo kabla ya kuelekea Amerika mwezi ujao. Viwanja vitakavyojengwa vitakuwa vya umma.

Serikali ilitengea Tennis Kenya ekari 10 za shamba mwaka 2015 katika kituo cha kimataifa cha michezo cha Kasarani. Shirikisho hilo lilisaini stakabadhi muhimu na shirika la kusimamia viwanja nchini (Sports Kenya) mwaka 2021.

“Tennis Kenya imetafuta fedha za kujenga viwanja viwili vya kwanza katika kituo hicho cha viwanja 24,” shirikisho hilo limesema na kushukuru Mungu kwa umbali limetoka na pia kutumai miaka 100 ijayo itakuwa ya baraka.

Itakuwa pia sherehe ya kubariki na kumpa kwaheri bingwa wa tenisi ya haiba ya Wimbledon ya wachezaji wawili kila upande ya chipukizi Okutoyi atakayejiunga na Chuo Kikuu cha Auburn kuendeleza tenisi na masomo.

You can share this post!

Moraa ni miongoni mwa 7 waliopokea tuzo ya heshima kutoka...

CHAKULA KITAMU: Ongeza pilipili na krimu kwa dagaa

T L