• Nairobi
  • Last Updated December 5th, 2023 10:25 PM
Vihiga Queens kileleni licha ya sare

Vihiga Queens kileleni licha ya sare

Na JOHN KIMWERE

VIHIGA Queens ingali kileleni mwa jedwali la Ligi Kuu ya Soka ya Wanawake licha ya kutoka sare tasa na Gaspo Women ugani Mumias Complex.

Nao mabingwa watetezi, Thika Queens ilijikuta kwenye wakati mgumu ilipozabwa bao 1-0 na Ulinzi Starlets ugani Ruaraka, Nairobi.

Mechi hiyo ilianza vyema huku Ulinzi Starlets ya kocha, Joseph Wambua ilionyesha soka safi ndani ya kipindi cha kwanza.

Ulinzi chini ya nahodha Diana Shakava, ilipoteza nafasi mbili safi kupitia Emily Auma aliyechanja mkwanju wa penalti dakika ya 18.

Dakika saba baadaye naye Landline Aoko alipoteza nafasi ya wazi alipobakia na kipa lakini wapi alishindwa kujuma ngozi ya ng’ombe ndani ya wavu.

Sawa na wapinzani wao Thika Queens chini ya kocha, Bertha Achieng itajilaumu baada ya Stella Adhiambo kupoteza nafasi mbili za wazi.

Ulinzi ilipata bao la ushindi kupitia juhudi zake Lucy Akoth kunako dakika ya 78.

”Ninashukuru Mungu kwa baraka zake. Amenibariki na mtoto kijana pia wachezaji wangu wamenipa ushindi mtamu wa alama tatu muhimu kwenye mechi zetu,” kocha wa Ulinzi alisema na kutoa wito kwa vipusa wake kuendeleza mtindo kwenye juhudi za kuwania taji hilo.

Kocha wa Ulinzi Starlets, Joseph Wambua akiongea na wachezaji wake wakati wa mechi yao dhidi ya Thika Queens ya Ligi Kuu ya Soka ya Wanawake (KWPL) walipobeba ushindi wa bao 1-0 ugani Ruaraka, Nairobi. PICHA | JOHN KIMWERE

Kwenye matokeo mengine ya mechi hizo, Kangemi Starlets kwa mara nyingine iliteleza na kushindwa kusajili ushindi wa kwanza ilipozabwa mabao 4-3 na Zetech Sparks, Wadadia iliandikisha ushindi wa mabao 2-0 mbele ya Kayole Starlets huku Bunyore Starlets ikidungwa bao 1-0 na Kisumu Allstarlets.

Nazo Trans Nzoia Falcons na Nakuru City Queens ziliumiza nyasi bure baada ya kutoka nguvu sawa kwa sare tasa.

MATOKEO YOTE

Ulinzi Starlets 1-0 Thika Queens

Vihiga Queens 0-0 Gaspo Women

Kisumu Allstarlets 1-0 Bunyore Starlets

Kangemi Starles 3-4 Zetech Sparks

Transnzoia Falcons 0-0 Nakuru City Queens

Wadadia 2-0 Kayole Starlets

  • Tags

You can share this post!

Ligi Kuu: KCB FC yapiga hatua baada ya kung’ata...

Mwalimu ashtakiwa kudai kinara wa TSC amekufa

T L