• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 6:50 AM
Wakala wa Lukaku atishiwa maisha kwa kufanikisha uhamisho wa nyota huyo hadi Chelsea

Wakala wa Lukaku atishiwa maisha kwa kufanikisha uhamisho wa nyota huyo hadi Chelsea

Na MASHIRIKA

FEDERICO Pastorello ambaye ni wakala wa fowadi Romelu Lukaku, amekiri kutishiwa maisha pamoja na familia yake wakati alipokuwa akifanikisha uhamisho wa sogora huyo raia wa Ubelgiji hadi Chelsea kwa Sh15.2 bilioni.

Lukaku, 28, aliagana na Inter Milan wiki hii baada ya kusaidia kikosi hicho cha Ligi Kuu ya Italia (Serie A) kunyanyua taji la kipute hicho kwa mara ya kwanza tangu 2009-10. Taji hilo lilikuwa la 19 kwa Inter kujizolea katika historia ya soka ya Italia.

“Kuna gumzo kwamba uhamisho wa Lukaku ulichochewa na tamaa ya pesa. Kuna madai ya kupotosha kwamba mchakato wa kuhama kwake “kulisukwa” na “kulazimishiwa” kwa ajili ya pesa,” akasema Pastorello.

“Nimepokea vitisho na familia yangu pia kutishiwa maisha. Hata hivyo, hatutatetereka. Tutakubali ukosoaji ambao una mashiko,” akaongeza.

Lukaku alifungia Inter Milan jumla ya mabao 64 kutokana na mechi 95 ambazo alichezea kikosi hicho katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Uhamisho huo ulimfanya Lukaku ambaye ni mfungaji bora wa muda wote kuwa sogora ghali zaidi kuwahi kuuzwa na kikosi cha Serie A.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO 

You can share this post!

Liverpool tayari kurefusha mkataba wa kiungo na nahodha...

De Bruyne, Foden kutochezea Man-City dhidi ya Spurs