• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 6:40 PM
Wanabunduki kwenye mizani ya Brighton leo Jumamosi

Wanabunduki kwenye mizani ya Brighton leo Jumamosi

NA MASHIRIKA

LONDON, Uingereza

ARSENAL watakabiliwa na mtihani mkali katika kampeni yao ya kusalia juu ya Ligi Kuu ya Uingereza watakapozuru uga wa Amex kuvaana na Brighton & Hove Albion, leo Jumamosi.

Vijana hao wa kocha Mikel Arteta wamedondosha alama katika michuano miwili pekee ligini msimu huu.

Wanabunduki hao wanakutana na wasumbufu Seagulls ambao wanaonekana kuwa wagombeaji halisi wa tiketi ya kushiriki mojawapo ya mashindano ya Bara Ulaya.

Seagulls wako na alama moja pekee nje eneo la kufuzu kushiriki Ligi ya Europa Conference.

Arsenal wanapigiwa upatu kukomoa Brighton. Hata hivyo, Brighton pia si wachache kwa sababu wanafukuzia ushindi wa pili mfululizo dhidi ya wanabunduki katika mashindano yote.

Vijana wa Arteta wametatizika katika safari zao uwanjani Amex tangu Brighton wapandishwe ngazi msimu 2016-2017.

Wawili hawa tayari wamekutana msimu ambapo Arsenal walibanduliwa kwenye kipute cha Carabao Cup. Brighton baadaye waliaga mashindano hayo katika raundi iliyofuata dhidi ya Charlton Athletic kwa njia ya penalti kabla ya kutandaza soka safi wakinyamazisha Southampton.

Kwa upande wao, Arsenal wana motisha baada ya kutoka nyuma wakilipua West Ham katika mechi ambayo Martin Odegaard, Gabriel Martinelli na Eddie Nketiah walisakata soka ya kupendeza.

Arsenal hawana nafasi ya kuteleza kwani mabingwa watetezi Manchester City wako alama tano pekee nyuma.
City inayojivunia kuwa na ‘muuaji’ Erling Haaland itapimwa na Everton uwezo wake.

Leo Jumamosi pia itakuwa zamu ya ‘mbwa mwitu’ wa Wolverhampton Wanderers kualika ‘mashetani wekundu’ wa Manchester United ugani Molineux.

Majirani Manchester City na Manchester United wataanza mechi zao na asilimia kubwa ya kutwaa ushindi, ingawa wapinzani wao hawawezi kudharauliwa.

Ratiba ya leo:

  • Wolves v Manchester United
  • Bournemouth v Crystal Palace
  • Fulham v Southampton
  • Manchester City v Everton
  • Newcastle v Leeds
  • Brighton v Arsenal
  • Tags

You can share this post!

Wandani wa Raila wakataa wito wa Mudavadi waunge serikali

Ripoti: Ufisadi wazidi kuongezeka nchini

T L