• Nairobi
  • Last Updated May 10th, 2024 5:50 AM
Wanariadha maarufu wa kikosi cha Marathon wajiondoa Team Kenya

Wanariadha maarufu wa kikosi cha Marathon wajiondoa Team Kenya

BERNARD ROTICH NA JOHN ASHIHUNDU

WANARIADHA kadhaa maarufu wa mbio za marathon wamejiondoa katika kikosi Kenya kitakachoshiriki katika Mashindano ya Dunia yatakayofanyika jijini Budapest, Hungary.

Bingwa wa London Marathon Kelvin Kiptum na Brigid Kosgei anayeshikilia rekodi ya Dunia kwa upande wa wanawake ni miongoni mwa waliojiondoa katika mashindano hayo yatakayoanza Agosti 19 na kumalizika Agosti 27.

Bingwa mara tatu wa half marathon, Geoffrey Kamworor pia amejiondoa kutoka kikosi hicho cha Team Kenya.

Titus Kipruto aliyeorodheshwa wa nne mwaka huu katika mbio za Tokyo Marathon ndiye pekee aliyebakia, huku nafasi za waliojiondoa zikijazwa na wanariadha walikuwa katika kikosi cha akiba.

Kipruto sasa ataungana na Timothy Kiplagat aliyemaliza wa pili katika Rotterdam Marathon na Joshua Belet aliyetwaa nishani ya fedha katika mbio za Hamburg Marathon.

Awali, Kiplagat alikuwa mkimbiaji wa akiba, wakati hii ikiwa mara ya kwanza kwa Belet kujumuisha kwenye timu hiyo.

Akitangaza mabadiliko hayo, Mkurugenzi wa idara ya mashindano katika shirikisho la Riadha Kenya, Paul Mutwi alisema Michael Gitahe anayeshikilia nishani ya shaba ya Michezo ya Jumuiya ya Madola atabakia kuwa mkimbiaji wa akiba.

Mutwi aliyetangaza mabadiliko hayo jana mjini Eldoret alisem Bethwel Kibet, aliyemaliza katika nafasi ya tano wakati wa Seville Marathon mnamo Februari ataungana na Githae wenye orodha ya wakimbiaji wa akiba.

Kiptum aliyeandikisha muda wa pili bora wakati wa London Marathon na Kamworor aliye bingwa mara mbili katika mbio za nyikani duniani walikuwa wamejmuishwa kwenye kikosi cha Team Kenya kilipotajwa June 2.

Kadhalika Shila Chepkirui anayeshikilia nishani ya fedha ya Olimpiki za Tokyo 2020 na kumaliza wa nne katika mbio London Marathon pia ameondolewa katika kikosi cha wanawake.

Sally Chepyegon Kaptich mshindi wa Barcelona Marathon aliyekuwa katika kikosi cha akiba pamoja na Shyline Jepkorir mshindi wa Enschede Marathon wamechukuwa nafasi za Kosgei na Chepkirui.

Wameungana na Margaret Wanjiru, mshindi wa Tokoyo Marathon zilizofanyika mwaka huu.

Mshindi wa nishani ya fedha, Margaret Wangari atabakia kuwa mkimbiaji wa akiba pamoja na Betty Chepkwony, bingwa wa Rome Marathon.

Watakaowakilisha Kenya kule Budapest ni, wanaume: Titus Kipruto (2:04;54), Timothy Kiplagat (2:03.50), Joshua Belet (2:04;33). Wakimbiaji wa akiba :- Michael Githae (2:07;28).

Wanawake: Rosemary Wanjiru (2:16;28), Sally Chepyegon Kaptich (2:20;03), Shline Jekorir (2:22;45). Wakimbiaji wa akiba: Margaret Wangari (2:23;52), Betty Chepkwony (2:23;02).

  • Tags

You can share this post!

West Ham watibua jaribio la kwanza la Arsenal kumsajili...

Ukimwi: Wajawazito Kilifi washauriwa kuhudhuria kliniki...

T L