• Nairobi
  • Last Updated May 14th, 2024 6:26 PM
Wasimamizi wapya wa Ligi Kuu kuteuliwa leo

Wasimamizi wapya wa Ligi Kuu kuteuliwa leo

Na JOHN ASHIHUNDU

KAMATI Simamizi ya Soka inayoongozwa na Jaji Mstaafu Aaron Ringera, itakutana na viongozi wa klabu za Ligi Kuu Nchini (KPL) na kuteua kampuni itakayosimamia mechi za ligi, hii leo.

Mkutano huo utakaofanyika asubuhi katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo mjini Nairobi, unatarajiwa kujaa mihemko ya aina yake huku klabu zikitoa kauli zao kuhusu usimamizi wa mechi za soka nchini.

Aidha, kampuni ya Kenyan Premier League (KPL) ni miongoni mwa zinazofikiriwa kupewa jukumu hilo la kuendesha kandanda ya Kenya, baada ya Shirikisho la Soka Kenya (FKF), lililokuwa likitekeleza wajibu huo, kuvunjiliwa mbali majuma chache yaliyopita kufuatia madai ya ufisadi.

Ali Amour – ambaye ni mwanachama katika kamati hiyo ya muda ya Ringera – alithibitishia Taifa Leo hapo jana kwamba, kamati hiyo iliyoteuliwa na serikali kusimamia shughuli za soka kwa miezi sita pia itajadili mipango ya kurejelewa kwa mechi za ligi zilizosimamisha kwa wiki mbili.

Mkutano huu unatokea siku chache tu baada ya kamati hiyo kutangaza kwamba inakutana na madhamini kadhaa kuona jinsi wanavyoweza kusaidia timu za ligi hizo kuendelea kucheza mechi zao chini ya Katiba Mpya ya Michezo.

Serikali kupitia kwa Waziri wa Michezo iliteua kamati ya Ringera kuendesha maswala ya soka nchini kabla ya uchaguzi kufanyika ili viongozi wapya kuchukue usukani na kupiga marufuku ligi kubwa za KPL, Supa Ligi (NSL), Ligi Kuu ya Wanawake na ile ya Daraja la Kwanza.

FKF-PL imekuwa ikiendeshwa na kamati ya Mwendwa tangu inyakue mamlaka hayo mwaka uliopita kwa njia ya mkato.KPL iliundwa mnamo 2003 na kupewa mamlaka ya kusimamia ligi kuu kuanzia 2015 hadi Septemba 24, 2020, lakini kutokana na kuzuka kwa maradhi ya corona haikuweza kuendesha shughuli hiyo hadi mwisho.

Katika mchanganyiko huo, Mwendwa alisimamisha msimu wa 2019/20 mnamo Aprili 2020 na kutawaza Gor Mahia kama mabingwa wa msimu huo, huku akipandisha klabu za City Stars na Bidco United kutoka Supa Ligi (NSL).

Hatua hiyo izua malalamishi kutoka kwa KPL ambao walisisitiza kwamba kama wasimamizi wa ligi kuu ndio waliotarajiwa kutoa muelekeo kuhusu ligi hiyo.Pamoja na klabu ya Chemelil Sugar KPL waliwasilisha kesi katika Mahakama ya Kutatua Mizozo ya Spoti (SDT) ya John Ohaga ambaye aliitupilia mbali kesi hiyo.

FKF ilichukua rasmi uendeshaji wa ligi kuu baada ya Mwendwa kutamatisha rasmi kandarasi ya kampuni hiyo.Kwa kipindi kirefu, pameshuhudiwa mizozo ya mara kwa mara kati KPL na FKF kiasi cha kuathiri makuzi ya maendeleo ya mchezo huo.

Kwa mujibu wa kandarasi ya 1015, KPL walikuwa na mamlaka ya kusimamia uendeshaji wa ligi hiyo hadi Septemba 24, 2020

You can share this post!

Voliboli: Tupo ng’ang’ari kutetea taji letu...

Jamaa, marafiki kiini cha masaibu ya wanariadha

T L