• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 7:47 PM
Voliboli: Tupo ng’ang’ari kutetea taji letu – kocha GSU

Voliboli: Tupo ng’ang’ari kutetea taji letu – kocha GSU

Na JOHN KIMWERE

KOCHA wafalme wa voliboli nchini GSU (jezi nyekundu), Gideon Tarus, amesema ameandaa vijana wake tayari kuanza kampeni za kutetea taji la Ligi Kuu muhula mpya.

Anasema anafahamu wazi kuwa kampeni za ngarambe hiyo hazitakuwa rahisi hasa baada ya kupata ushindani mkali kwenye mechi za msimu uliyopita. Kwenye juhudi za kujiweka imara kikosi hicho kimenasa huduma za mvamizi Joshua Kimaru aliyekuwa akipigia Equity Bank.

GSU ilisajili mchezaji huyo ili kujaza pengo lililokuwa limeachwa wazi na Cornelius ‘Nder’ Kiplagat aliyekuwa asajiunge na El Gaish ya Misri. Hata hivyo dili yake haikufaulu ambapo amerejea kuendelea kuhudumia timu yake.

”Sina shaka kutaja kuwa Kimaru ana uwezo wa kufaulu kuteuliwa katika kikosi cha kwanza,” alisema na kuongeza kuwa endapo hatapata timu nyingine watatumia huduma za wote wawili. GSU itatetea kombe la taji hilo baada ya kulishinda kwa mara ya tatu mfululizo msimu uliyopita kwenye mechi zilizopigiwa ukumbi wa Makande, Mombasa.

GSU ilibeba ubingwa huo baada ya kulaza wapinzani wengine Kenya Prisons, Halmashauri ya Bandari ya Kenya (KPA) na Jeshi la Ulinzi (KDF). Kampeni za muhula mpya zimepangwa kukunjua jamvi Ijumaa wiki hii.

You can share this post!

Kitaumana leo Etihad

Wasimamizi wapya wa Ligi Kuu kuteuliwa leo

T L