• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 8:55 PM
Watford wasajili kiungo Louza wa Nantes kadri wanavyojisuka upya kwa msimu ujao wa 2021-22 kwenye EPL

Watford wasajili kiungo Louza wa Nantes kadri wanavyojisuka upya kwa msimu ujao wa 2021-22 kwenye EPL

Na MASHIRIKA

WATFORD wamemsajili kiungo mahiri mzawa wa Ufaransa na raia wa Morocco, Imran Louza kutoka kambini mwa FC Nantes ya Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) kwa mkataba wa miaka mitano.

Louza anatua ugani Vicarage Road kwa kima cha Sh1.4 bilioni baada ya kufungia Nantes jumla ya mabao saba kutokana na mechi 35 za Ligue 1 mnamo 2020-21.

Japo aliwahi kuwakilisha Morocco katika mashindano kadhaa ya chipukizi wasiozidi umri wa miaka 17 na 19, Louza alihiari kuvalia jezi za Ufaransa na amekuwa sehemu ya kampeni za kikosi cha U-21 nchini humo.

Louza aliingia katika sajili rasmi ya Nantes akiwa na umri wa miaka minane na amechezea kikosi hicho mara 58 tangu awajibishwe kwa mara ya kwanza mnamo Januari 2019.

Anakuwa mchezaji wa pili baada ya beki Mattie Pollock aliyetokea Grimsby Town kusajiliwa na Watford waliopandishwa ngazi kutoka Ligi ya Daraja la Kwanza (Championship) mwishoni mwa msimu wa 2020-21 hadi Ligi Kuu ya Uingereza (EPL). Pollock alisajiliwa na Watford kwa kima cha Sh35 milioni.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

NGILA: Nchi za Afrika ziungane kujiendeleza kiteknolojia

WASONGA: Muturi asalie msemaji wa Mlimani, asiwanie urais...