• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Zetech yazidi kuwika kwenye karate

Zetech yazidi kuwika kwenye karate

THIKA.

Na LAWRENCE ONGARO

MASHINDANO ya Skai Kenya Opens yalifanyika mjini Thika, mwishoni mwa wiki huku matayarisho hayo yakiendeshwa na chama cha karate cha Shoto Kan karate Alliance International.

Klabu 12 za karate, zilishiriki huku klabu ya Zetech ikitawazwa mshindi baada ya kuzibwaga klabu zote zilizoshiriki. Klabu ya Zetech ilizoa jumla ya medali 13, huku ikijivunia dhahabu sita, fedha sita na shaba moja.

Kocha wa Zetech anaelezea kuwa bidii na unyenyekevu ndiyo ilifanya kuibuka na ushindani mkubwa hivyo. Klabu ya pili Dilpak ilikamata nafasi ya pili na jumla ya pointi 10. Klabu ya Thika Brook ni ya tatu ikikamata pointi 14. Ilizoa dhahabu 4, fedha 8 na Shaba 2

Klabu ya Fursa Kenya ilikuwa ya nne na dhahabu 4, fedha 2 na Shaba 5. ilipata pointi 11 huku klabu ya Kick master ikifunga tano bora ikipata pointi 16 na dhahabu 3 fedha 6 na Shaba 7. Klabu ya South Coast iliibuka nafasi ya sita na dhahabu 2 na Shaba 5 wakizoa pointi 7.

Chuo cha JKUAT ya Juja kilikamata nafasi ya saba na dhahabu moja na Shaba 2 huku wakizoa pointi 3 pekee. Klabu ya Kirwara na Machakos na Murang’a, zilipata Shaba moja kila moja na pointi 1. Halafu chuo cha Chuka university na Parklands zilitoka mikono tupu bila kupata medali yoyote.

Kocha wa Zetech Martin Ndegwa aliisifu klabu yake Alisa walifanya mazoezi makali Kwa mwezi moja mfululizo huku vijana wake wakifuata maagizo yake. ” Nimerithika na jinsi vijana wangu walicheza na hiyo ni dhihirisho kuwa klabu ya Zetech bado ni mabingwa wa karate,” alijitetea kocha huyo.

Amewahimiza vijana wake wasilegeze kamba bali waendelee kuzingatia mazoezi.

You can share this post!

Chui, Blades mabingwa Hoki ya taji la Easter

‘ Wajungle’ kuwania ugavana na tikiti ya...

T L