• Nairobi
  • Last Updated May 13th, 2024 9:17 PM
Gachagua asema wawaniaji huru wanaongozwa na ubinafsi

Gachagua asema wawaniaji huru wanaongozwa na ubinafsi

MBUNGE wa Mathira Rigathi Gachagua ambaye ni mgombeaji mwenza wa Naibu Rais Dkt William Ruto amewakashifu wanasiasa waliohama UDA baada ya mchujo kisha kuamua kuwania kama wagombeaji huru.

Bw Gachagua alisema kuwa iwapo wawaniaji hao wana imani katika demokrasia basi wanastahili kuwaunga mkono wale ambao waliwabwaga katika mchujo wa chama hicho.

“Wawaniaji huru ni watu ambao wana ubinafsi na wanasukumu tu ajenda yao bila sera maalum. Hapa Baringo tutawafanyia kampeni wale ambao wanawania kupitia UDA pekee,” akasema Bw Gachagua katika mkutano wa kisiasa Kaunti ya Baringo.

Kwa mara nyingine, alikariri kuwa wakazi wa Mlima Kenya watampigia Dkt Ruto kura kisha kuwachagua tu wale wanaowania kupitia UDA.

“Iwapo hamtawapigia wawaniaji wa UDA kura, Dkt Ruto atakuwa jemedari bila majeshi yake. Lazima mhakikishe mnawachagua watu ambao wapo tayari kufanya kazi na chama. Kama watu wa Mlima Kenya wamekubali kuwachagua wawaniaji wa UDA, kwa nini hapa mwachague wagombeaji huru?” akasema Mbunge huyo wa Mathira.

Kauli yake ilionekana kuwalenga Gavana wa sasa Stanley Kiptis na mbunge wa Eldama Ravine Moses Lessonet ambao wameamua kuwania kiti cha ugavana kama wawaniaji huru baada ya kubwagwa na Benjamin Cheboi.

  • Tags

You can share this post!

Utalii: Balala awataka wawekezaji kusaka soko jipya

Waziri atimuliwa baada ya watoto 11 kuteketea

T L