• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 9:16 PM
Kioni: UDA ilichezea Jubilee rafu Mlimani

Kioni: UDA ilichezea Jubilee rafu Mlimani

KATIBU Mkuu wa Jubilee Jeremiah Kioni mnamo Ijumaa alidai chama cha United Democratic Alliance (UDA) kilishinda viti vingi katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9 kutokana na kile alichotaja kama “siasa za utoaji hongo”.

“Tulishuhudia visa vingi vya kuhongwa kwa wapiga kura. Tuliumia kwa kutoshiriki uovu huu na ndiposa tukapoteza viti vyetu,” akasema.

Hata hivyo, hakutoa ushahidi wowote kuthibitisha madai yake.

Bw Kioni alishindwa kuhifadhi kiti chake cha ubunge wa Ndaragua kwa kulemewa na mgombeaji wa chama cha UDA George Gachagua aliyezoa jumla ya kura 30,180 huku akipata kura 7,227.

Hata hivyo, Bw Kioni alisema yeye na chama cha Jubilee hawajakerwa na kushindwa kwao lakini walisimama kidete na maadili na sera ambazo waliamini kwazo.

Lakini Gavana mteule wa Murang’a Irungu Kang’ata alipuuzilia mbali madai ya Bw Kioni akisema “yanatokana na hasira za kushindwa.”

“Ningependa kumhakikishia Bw Kioni kwamba wapiga kura wa Mlima Kenya walienda debeni kujinasua kutoka kwa utawala wa kidikteta wa Jubilee,” akasema Bw Kang’ata ambaye hadi kuchaguliwa kwake alikuwa Seneta wa Murang’a.

  • Tags

You can share this post!

Magoha asogeza tarehe ya wanafunzi kurudi shuleni

Brentford yadhalilisha Manchester United katika EPL

T L