• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 7:50 AM
Kura ya maoni yamweka Raila mbele ya Ruto jijini Nairobi

Kura ya maoni yamweka Raila mbele ya Ruto jijini Nairobi

NA LEONARD ONYANGO

MWANIAJI wa muungano wa Azimio la Umoja One Kenya, Raila Odinga atazoa kura nyingi jijini Nairobi iwapo Uchaguzi Mkuu utafanyika leo.

Ripoti ya utafiti wa kura za maoni uliofanywa na shirika la Trends and Insights Africa (Tifa) inaonyesha kuwa asilimia 41 ya wakazi wa Nairobi watapigia kura Bw Odinga nao asilimia 26 watapigia kura Naibu Rais William Ruto.

Ikiwa utafiti huo unaashiria hali halisi, basi Bw Odinga ataendeleza ubabe wake wa kudhibiti jiji la Nairobi tangu 2013.

Katika uchaguzi wa 2013, Bw Odinga alipata asilimia 49 ya kura za Nairobi huku Rais Uhuru Kenyatta wa Jubilee akifuatia kwa asilimia 47.

Katika Uchaguzi wa Agosti 8, 2017 ambao matokeo yake ya urais baadaye yalibatilishwa na Mahakama ya Juu, Bw Odinga alikuwa amepata kura 828,826 huku Rais Kenyatta akiwa na kura 791,291.

Katika uchaguzi wa 2017, chama cha ODM kilishinda viti vinane vya ubunge jijini Nairobi kati ya 17.

Chama cha Jubilee pia kilishinda viti vinane huku Wiper kikinyakua kimoja.

Kati ya wadi 85, ODM ilishinda udiwani katika wadi 40 huku Jubilee ikinyakua wadi 45.Raila pia atachukua kura zaidi ukifanyika leo katika kaunti za Mombasa na Makueni.

Kuhusu kiti cha ugavana jijini Nairobi, utafiti huo unasema Johnson Sakaja atambwaga Polycarp Igathe uchaguzi ukiandaliwa leo.

  • Tags

You can share this post!

Wazazi wanaoingiza wana wao sekondari walia kukabiliwa na...

Jinsi walivyojifunga jela kwa kuabiri basi la Azimio

T L