• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 5:10 PM
Mahakama ya juu yampa Tuju afueni ya muda

Mahakama ya juu yampa Tuju afueni ya muda

NA SAM KIPLAGAT

MAHAKAMA ya Upeo imempa afueni kuu aliyekuwa waziri Bw Raphael Tuju kwa kusitisha kupigwa mnada kwa mali yake mtaani Karen kutokana na deni la Sh2.2 bilioni analodaiwa na benki ya kanda.

Majaji watano wa Mahakama ya Upeo wamesimamisha kutwaliwa kwa mali ya Tuju na benki ya East African Development Bank (EADB) hadi kesi aliyowasilisha waziri huyo wa zamani isikilizwe na kuamuliwa.

Majaji hao walikubaliana na ombi la Bw Tuju kwa sababu uamuzi wa Mahakama ya Rufaa iliibua sheria ya Maamuzi ya nchi za Kigeni, ambayo inaruhusu kutambuliwa kwa maamuzi yaliyotolewa ng’ambo, kuhusu sheria za Kenya na katiba.

Bw Tuju pia alidai kwamba hakupatiwa nafasi ya kujitetea katika korti za Uingereza inavyohitajika kisheria na kwamba Mahakama ya Rufaa ilipuuza utetezi wake.

Hatua hiyo inajiri siku chache baada ya Mahakama ya Rufaa kutupilia mbali kesi ya Bw Tuju aliyopinga kutekelezwa kwa uamuzi wa korti ya Uingereza kuhusu deni hilo na kutoa nafasi kwa mali yake kupigwa mnada na madalali.

  • Tags

You can share this post!

Ahadi ya Ruto kuhusu bei ya unga sasa yatamausha

Sakaja kutimua wafanyakazi 715 waliokuwa wameajiriwa na NMS

T L