• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 1:05 PM
Masuala tisa yaliyozima kesi ya Raila katika Mahakama ya Upeo

Masuala tisa yaliyozima kesi ya Raila katika Mahakama ya Upeo

NA RICHARD MUNGUTI

UAMUZI wa kesi ya kupinga matokeo ya kura za urais uliegemea zaidi juu ya masuala tisa yaliyotambuliwa yenye kuzua utata na ambayo majibu yake yalimdungua siasani kinara wa muungano wa Azimio La Umoja-One Kenya Raila Odinga.

Jaji Mkuu Martha Koome pamoja na Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu, Mohammed Ibrahim, Smokin Wanjala, Njoki Ndung’u, Isaac Lenaola na William Ouko walichomoka kutoka faraghani Jumatatu kuamua ikiwa Dkt William Ruto alichaguliwa kihalali kuwa rais au la.

Bw Odinga aliwasilisha kesi kupinga matokeo ya urais kufuatia uchaguzi mkuu wa Agosti 9, 2022 ambapo Dkt Ruto alitangazwa mshindi baada ya kuzoa kura 7, 176,141 huku Bw Odinga akipata kura 6,942,930.

Baada ya kuwasilishwa kwa kesi nane za kupinga matokeo ya kura za urais majaji wa Mahakama ya Upeo walitambua masuala tisa waliyoyazingatiwa wakati wa kutolewa kwa uamuzi.

Masuala hayo ni: –

1.Ikiwa mitambo ya kiteknolojia almaarufu Kiems iliyotumika kuwatambua wapiga kura na kupeperusha matokeo ya uchaguzi wa Agosti 9 ilifikia ubora hitajika

2.Ikiwa utumaji wa matokeo ya uchaguzi kwa mtandao wa IEBC ulivurugwa

3.Ikiwa Fomu 34A zilizotumwa katika mtandao wa IEBC zilikuwa tofauti na zile zilizopewa maafisa wa kusimamia uchaguzi katika vituo vya kupigia kura pamoja na zile zilizopewa maajenti wa wawaniaji wa urais vituoni

4.Ikiwa kuahirishwa kwa uchaguzi wa Magavana katika kaunti za Kakamega na Mombasa, pamoja na maeneo ya uwakilishi bungeni ya Kitui Rural, Kacheliba,Rongai na Pokot na Wadi ya Nyaki Magharibi eneo la uwakilishi bungeni la Imenti kaskazini na Wadi ya Kwa Njenga kuwanyima wapiga kura fursa ya kupiga kura za urais

5.Ikiwa kulikuwa na tofauti za kura zilizopigiwa wawaniaji wa kiti cha urais na nyadhifa zile nyingine za Ugavana, Useneta, Ubunge na Udiwani

6.Ikiwa IEBC ilikagua na kutathmini na kutangaza matokeo ya kura za urais kwa mujibu wa kifungu nambari 38(3) ©na 138(10) cha Katiba

7.Ikiwa rais mteul Dkt William Ruto aliyetangazwa na mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati alipata asili mia 50 + 1 ya kura zilizopigwa kulingana na Kifungu nambari 138 cha Katiba

8.Ikiwa kulikuwa na makosa ambayo yatapelekea kubatilishwa kwa matokeo ya kura za urais

9 Maagizo yanayopaswa kutolewa

Baada ya kuchambua ushahidi wote majaji hao saba walisema hakuna ushahidi uliowasilishwa na Bw Odinga na walalamishi wengine saba kuwezesha mahakama kutupilia mbali ushindi wa Dkt Ruto.

Uamuzi huo kwa kiwango fulani unaweza ukawa na athari ya kumstaafisha Bw Odinga katika siasa.

  • Tags

You can share this post!

Mahakama yasalia kimya kuhusu hatma ya kura za urais kutoka...

Shirika la We Don’t Have Time laendelea na shughuli...

T L