• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 5:50 AM
Mwaura hatimaye akubali matokeo ya mchujo Ruiru

Mwaura hatimaye akubali matokeo ya mchujo Ruiru

NA SIMON CIURI

SENETA Maalum, Isaac Mwaura hatimaye amekubali matokeo ya uchaguzi wa mchujo wa chama cha UDA katika eneobunge la Ruiru, Kaunti ya Kiambu.

Awali, Bw Mwaura alikuwa amekataa kukubali kushindwa na mbunge wa eneo hilo, Bw Simon King’ara, akidai kwamba shughuli hiyo ilikumbwa na udanganyifu.

Lakini jana Jumapili, Bw Mwaura alibadili msimamo wake alipokubali kumuunga mkono Bw King’ara kupeperusha bendera ya UDA kwenye uchaguzi wa Agosti 9.

Kulingana na matokeo ya shughuli hiyo, Bw King’ara alizoa kura 5, 747 huku Bw Mwaura akipata kura 2, 901. Eneobunge hilo lina zaidi ya wapigakura 200,000.

Alhamisi, Bw Mwaura alisema kuwa alipokonywa ushindi wake na kukitaka chama hicho kurudia uchaguzi huo.

Lakini mnamo Jumamosi usiku, Bw King’ara alikabidhiwa cheti cha ushindi wa chama hicho kwenye hafla iliyofanyika katika Taasisi ya Mafunzo ya Sayansi na Teknolojia ya Kiambu (KIST).

Wakati huo huo, mbunge Patrick Wainaina (Thika Mjini) amesema kuwa atawania ugavana wa kaunti hiyo kama mwaniaji huru.

  • Tags

You can share this post!

MWALIMU WA WIKI: Mdarisi mkwasi wa vipaji katika masomo ya...

MAKALA MAALUM: Njaa: Serikali imewasahau wakazi wa...

T L