• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 6:50 AM
Mwiraria: Waziri stadi na mweledi wa uchumi

Mwiraria: Waziri stadi na mweledi wa uchumi

KWA HISANI YA KENYA YEAR BOOK

DAVID, wengine walimwita tu Daudi- Mwiraria, mtaalamu wa miaka mingi na mwanasiasa ametajwa kuwa Waziri wa Fedha aliyefaulu sana baada ya Mwai Kibaki. Alifariki kutokana na saratani ya mifupa mwaka wa 2017.

Kibaki alimtaja Mwiraria aliyekuwa waziri wake wa fedha na mhadhiri mwenzake katika chuo kikuu cha Makerere kama “rafiki, mwandani, mfanyakazi mwenza na mshirika mwaminifu. Alisifu weledi wake katika masuala ya uchumi na umakinifu, unyenyekevu na uwazi.

“Aliheshimiwa kote bila kulazimisha. Kenya imempoteza mtumishi wa umma mwenye bidii ambaye lengo lake lilikuwa ni kutakia kila mtu mazuri. Roho yake ilale kwa amani ya milele” Kibaki alisema.Ilikuwa vigumu kutomheshimu Mwiraria, hata kama ulikuwa wa mrengo tofauti wa kisiasa na wake.

Kimo kifupi cha mwili wake kilifunikwa na werevu, ufahamu wa kina wa serikali na utumishi wa umma, na fauka ya yote, mamlaka na jinsi alivyokuza sera za uchumi na maendeleo kwa urahisi. Aliweza kwa kila kitu alichofanya. Kulikuwa na kitu kikubwa zaidi kumhusu Mwiraria.

Mbunge huyo wa Imenti Kaskazini kwa mihula mitatu alikuwa muungwana. Aliepuka siasa za matusi, uongo wa kuaibisha na siasa za za kumalizana. Badala yake alikuwa mwanasiasa asiyekuwa na pupa, alichagua kujitosa katika uwanja wa siasa ambapo wale wanaopaza sauti ya juu na wachafu wanapata wanachotaka.

Lakini Mwiraria, kumnukuu mwanafunzi mwenzake katika shule ya Wavulana ya Alliance, mwanahabari wa miaka mingi Philip Ochieng’, alikuwa “na akili iliyosoma”; mtaalamu aliyetumia maisha yake yote ya kazi akitunga na kutekeleza sera za serikali na kupima ukweli na takwimu.

Msikilize Raila Odinga: “Nilikuwa na heshima ya kufanya kazi na Mheshimiwa Mwiraria kama mbunge mwenzangu na baadaye kama wanachama wa baraza la mawaziri. Alikuwa mtumishi wa umma mwaminifu na mwenye bidii aliyeweka maslahi ya nchi ndani ya moyo wake.

“Nitakumbuka kazi tuliyofanya pamoja ya kubadilisha taasisi muhimu za serikali kama Mamlaka ya Ukusanyaji Ushuru, Ununuzi katika Umma, na ufadhili wa miundomsingi na utekelezaji wakati National Rainbow Coalition ilipoingia mamlakani 2002.

“Ni Mheshimiwa kujitolea na umakinifu wa Mwiraria kama waziri wa fedha ambao uliwezesha Narc kutimiza ahadi zake zote katika sekta muhimu za uchumi wakati ambao uchumi ulikuwa umeharibika.”Katika eneobunge la Imenti Kaskazini alilowakilisha kwa mihula mitatu, alijulikana kama Kangumu kwa sababu ya kutowapa watu pesa kama Kibaki.

Afisa mstaafu wa ujasusi Essau Kioni anaeleza kuwa Mwiraria, anayefahamika kwa matumizi mazuri ya pesa zake, aliamini watu wanafaa kufanya kazi kwa bidii na sio kutegemea kupatiwa pesa na viongozi. Kama waziri wa fedha, Mwiraria alikuwa nguzo ya mkakati wa Kibaki wa kufufua uchumi, lakini pia alikuwa kama Kibaki katika mambo mengi na mmoja wa washirika wake wa karibu na alioamini serikalini.

Wawili hao walijuana wakiwa Makerere hata kabla ya Kenya kupata uhuru.Mwiraria alikuwa katibu wa Kibaki katika wizara ya fedha 1992 na wakishirikiana na marafiki wa karibu sana walisaidia kuunda chama cha DP.

You can share this post!

TAHARIRI: Njaa haifai kusumbua miaka 58 tangu uhuru

Wapwani kweli wataungana kisiasa au ni ndoto ya mchana?

T L