• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 9:16 PM
Naibu Mwenyekiti wa ODM Kilifi apoteza kiti cha udiwani

Naibu Mwenyekiti wa ODM Kilifi apoteza kiti cha udiwani

NA ALEX KALAMA

NAIBU mwenyekiti wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM) kaunti ya Kilifi ambaye pia ni mwakilishi wa wadi ya Kakuyuni Nixon Mramba alishindwa kukihifadhi kiti chake baada ya kulemewa na mgombea wa chama cha United Democratic Alliance (UDA) Morris Hinzano Kitsao.

Mramba ambaye alikuwa anawania wadhifa huo kwa tiketi ya chama cha ODM alipata kura 1375 lakini akaibuka kuwa wa pili baada ya mgombea wa kiti cha udiwani wa eneo hilo kwa tiketi ya chama cha UDA kupata kura 1568.

Mwanasiasa huyo mwenye uzoefu mkubwa na ambaye pia amekuwa diwani wa Kakuyuni kwa muda wa miaka 20 mfululizo alikuwa anawania tena kiti hicho cha wadi ya Kakuyuni kwa tiketi ya chama cha ODM.

Mramba ni mmoja wa wanasiasa mashuhuru tena shupavu katika kaunti ya Kilifi hasa miongoni mwa kaya za Wamijikenda.

Hata hivyo Hinzano ambaye alikuwa akiwania kiti hicho kwa mara ya kwanza alieleza furaha yake na nia yake ya kuwatumikia kwa bidii wanainchi wa wadi ya Kakuyuni.

Katika wadi ya Kakuyuni jumla ya kura zilizosajiliwa ni 8750, halali 4578 na zilizokataliwa zikiwa 31.

Na katika wadi ya Ganda mwakilishi wa wadi ya Ganda Reuben Katana ambaye alikihama chama cha ODM na kujiunga na kile cha Pamoja African Alliance kinachoongozwa ni gavana wa Kilifi Amasoni Kingi alipoteza kiti chake kwa mgombea wa chama cha ODM Oscar Wanje baada ya kupata kura 1554 huku Oscar Wanje wa ODM akiibuka mshindi kwa kuzoa jumla ya kura 2981.

Jumla ya kura zilizosajiliwa katika wadi ya Ganda 18566, kura halali zikiwa ni 8792, kura zilizokataliwa zikiwa ni 94.

  • Tags

You can share this post!

ODM yapokonywa ubunge Ganze ubingwa ukimwendea Kenneth...

Kiunjuri ahimili mawimbi ya UDA Mlima Kenya kushinda ubunge

T L