• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 8:50 AM
Orengo aponda wabunge ‘waasi’ Azimio akisema wasukumwa na ubinafsi

Orengo aponda wabunge ‘waasi’ Azimio akisema wasukumwa na ubinafsi

NA WANDERI KAMAU

GAVANA James Orengo wa Siaya jana Jumamosi aliwakashifu vikali wabunge ‘waasi’ kutoka mrengo wa Azimio la Umoja ambao wametangaza ushirikiano wa kisiasa na Rais William Ruto, akiwafananisha na “watoto waliomtoroka mama yao”.

Bw Orengo alisema wanaosingizia kutafuta maendeleo kwa serikali wanapotosha kwa kuwa kuna utaratibu wa kisheria kuhusu namna fedha za serikali zinatumika.

Akihutubu kwa lugha ya Dholuo wakati wa mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Elimu, Profesa George Magoha, Bw Orengo aliwaambia wabunge hao kimafumbo kuwa, hata wakitoka Azimio na kuelekea katika mrengo wa Kenya Kwanza, bado wao ni ‘watoto’ wa Azimio.

Kauli yake iliwalenga baadhi ya wabunge katika vyama vya ODM na Jubilee ambao majuzi walikutana na Rais Ruto na Naibu Rais Rigathi Gachagua katika Ikulu ya Nairobi, ambapo walitangaza kuanzisha ushirikiano na serikali. Kiongozi wa ODM, Raila Odinga aliwataja “wasaliti”.

Kwenye kikao cha Azimio mnamo Alhamisi katika Ukumbi wa Maanzoni, Machakos, mbunge Phelix Odiwuor ‘Jalang’o’ wa Lang’ata alizuiwa kushiriki katika kikao hicho akilaumiwa kuwa ‘mpelelezi’ wa Kenya Kwanza katika Azimio.

Bw Odinga alisema lazima wabunge wawe na kibali cha uongozi wa vyama vyao kila wanapopanga kukutana na Rais.

Katika Jubilee, kumezuka makundi mawili, kundi moja likiongozwa na Katibu Mkuu Jeremiah Kioni na jingine ‘asi’ likiongozwa na mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Kanini Keega, ambaye ametangazwa kuwa Kaimu Katibu Mkuu katika hali tatanishi.

Wakati huo huo, Bw Orengo alieleza hofu kuwa Kenya inaelekea katika mfumo wa siasa za chama kimoja kufuatia hatua ya Rais Ruto ‘kuwanyakua’ wabunge wa upinzani.

  • Tags

You can share this post!

FATAKI: Usitoe huduma za mke wa ndoa kwa dume ambalo wala...

BAHARI YA MAPENZI: Ubunifu wahitajika kudumisha mvuto

T L