• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 10:59 AM
Raila atorokwa zaidi na wabunge wa ngome yake ya Luo Nyanza, Langata

Raila atorokwa zaidi na wabunge wa ngome yake ya Luo Nyanza, Langata

NA CHARLES WASONGA

RAIS William Ruto anaendelea kusambaratisha upinzani kwa kuvutia wabunge na maseneta wa vyama tanzu katika muungano wa Azimio la Umoja-One Kenya upande wake.

Mnamo Jumanne, Februari 7, 2023 alivamia chama cha ODM kinachoongozwa na kiongozi wa Azimio Raila Odinga kwa kutwaa wabunge sita na seneta mmoja.

Viongozi hao walimtembelea Dkt Ruto katika Ikulu ya Nairobi na kuapa kuunga mkono serikali yake ya Kenya Kwanza.

Wao ni wabunge: Gideon Ochanda (Bondo), Elisha Odhiambo (Gem), Mark Ogolla Nyamita (Uriri), John Walter Owino (Awendo), Paul Abuor (Rongo), Omondi Caroli (Suba Kusini) na Phelix Odiwuor almaarufu Jalang’o (Langata), wote waliochaguliwa kwa tiketi ya ODM.

Pamoja nao pia alikuwa Mbunge wa Kisumu Mjini Mashariki Shakeel Shabir ambaye alichaguliwa kwa tiketi huru na Seneta wa Kisumu Tom Ojienda (ODM).

“Ulikuwa ni mkutano mzuri na sisi kama wabunge tumehakikishia Rais na Naibu wake kwamba tunataka maendeleo wala sio siasa,” akasema Bw Odhiambo.

“Hatutaki kuhusishwa na vitendo vya kuvuruga amani nchini kupitia maandamano na mikutano ya kuchochea hisia kali na chuki. Wakati wa siasa uliisha baada ya uchaguzi mkuu wa Agosti 9, 2022 na sasa ni wakati wetu kama viongozi waliochaguliwa kuwahudumia raia,” akaongeza.

  • Tags

You can share this post!

Manchester City washtakiwa kwa kukiuka sheria za matumizi...

Ardhi jirani na ya Ruto yanyakuliwa Taita

T L