• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 3:24 PM
Raila kushiriki NDC ya Wiper

Raila kushiriki NDC ya Wiper

Na JUSTUS OCHIENG

KIONGOZI wa chama cha ODM Raila Odinga, leo anatarajiwa kuhudhuria kongamano la kitaifa la wajumbe wa chama cha Wiper Democratic Movement – ishara kwamba anaweza kushirikiana tena na Bw Kalonzo Musyoka, aliyekuwa mgombea mwenza wake katika uchaguzi mkuu wa 2013 na 2017.

Kituo cha Stephen Kalonzo Musyoka (SKM) Command Centre kinachoongoza kampeni za kiongozi huyo wa Wiper, jana kilithibitishia Taifa Leo kwamba Bw Odinga na vinara wenza wa One Kenya Alliance Musalia Mudavadi (Amani National Congress), Gideon Moi (Kanu) na Moses Wetang’ula (Ford Kenya) pamoja na wawakilishi kutoka chama cha Jubilee cha Rais Uhuru Kenyatta, wanatarajiwa katika kongamano hilo litakalofanyika katika uwanja wa michezo wa Kasarani, Nairobi.

Naibu Mwenyekiti wa Wiper Mutula Kilonzo Jnr, alifichua kuwa idhini ya kubuni miungano itakuwa moja ya ajenda za kongamano la leo.“Ajenda yetu ni kurekebisha Katiba (ya chama), rangi, kuteua maafisa wapya na kuidhinisha SKM (Stephen Kalonzo Musyoka) kuwa mwaniaji urais mnamo 2022.

Mapema mwaka huu, chama hicho kilitoa ilani ya kubadilisha jina na rangi zake kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.Itakuwa mara ya pili kwa Bw Odinga kuhudhuria NDC ya chama tanzu cha OKA baada ya kuhudhuria ya chama cha Kanu katika ukumbi wa Bomas of Kenya Septemba 30.“Hii itakuwa hafla kubwa.

Kila kitu kimependekezwa na kusimamiwa na SKM Command Center,” alisema mwanachama wa SKM Command Centre.“Kalonzo alikuwa amemwalika Rais Uhuru Kenyatta na chama chake cha Jubilee lakini tuko na habari kwamba rais anaweza kutuma watu wake kutoka chama cha Jubilee.

”Mnamo Jumanne, Bw Musyoka aliongoza mkutano muhimu wa chama kabla ya kongamano la leo.Kongamano hilo linajiri siku mbili baada ya OKA na Mt Kenya Unity Forum kuanza kusuka muungano ambao huenda ukawa mrengo wa tatu katika uchaguzi mkuu wa 2022.

You can share this post!

Wahanga wa ghasia za 2007 wafidiwe kabla ya Uhuru kutoka...

Watavuruga hesabu za Raila, Ruto?

T L