• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 9:50 AM
Ruto asihi ngome yake kuwakataa wawaniaji wasio wa chama chake

Ruto asihi ngome yake kuwakataa wawaniaji wasio wa chama chake

FRED KIBOR

KWA siku ya pili mfululizo, Naibu Rais William Ruto amewalilia wakazi wa ngome yake wasimuaibishe Jumanne ijayo kwa kuchagua wasiokuwa wa chama chake cha United Democratic Alliance (UDA).

Akionekana kukabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa waliopoteza kwenye mchujo wa UDA, Dkt Ruto aliwataja viongozi hao kuwa “maadui”.

“Nimezunguka nchi nzima na UDA ndicho chama mashuhuri. Msiniaibishe hapa nyumbani kwa kuchagua watu ambao si wa UDA au muungano wa Kenya Kwanza. Baadhi ya viongozi walioungana dhidi yangu wanawania kama wagombea huru. Nawaomba tafadhalini muwakatae,” akasema Jumatatu katika Kaunti ya Nandi.

Dkt Ruto alikuwa ametoa kauli kama hiyo akiwa Eldoret na Baringo, ambapo alihimiza wakazi wapige kura kwa mfumo wa suti kamili (yaani kuanzia rais hadi MCA wa UDA au Kenya Kwanza).

Katika kaunti ya Nandi kuna wabunge watano waliotemwa ambao ni Vincent Tuwei (Mosop), Cornelly Serem (Aldai), Alfred Keter (Nandi Hills) na Wilson Kogo (Chesumei) ambao sasa ni wagombea huru.

Uasin Gishu kuna Swarup Mishra (Kesses), Sila Tiren (Moiben) na William Chepkut (Ainabkoi) wanaotetea nyadhifa zao wakiwa huru. Pia, mfanyibiashara Zedekiah Bundotich (Buzeki) anawania ugavana dhidi ya Jonathan Bii (Koti Moja) kutaka ugavana akiwa huru.Gavana wa Baringo Stanley Kiptis pia anamkabili Benjamin Cheboi wa UDA.

  • Tags

You can share this post!

Ipsos: Raila kifua mbele huku zikisalia siku 6

TAHARIRI: Uamuzi wa kufunga shule ghafla hakika utatatiza...

T L