• Nairobi
  • Last Updated May 10th, 2024 9:50 AM
Ruto atarajiwa Pwani wandani wakizozana

Ruto atarajiwa Pwani wandani wakizozana

NA WINNIE ATIENO

NAIBU Rais William Ruto anazuru Pwani leo Jumanne, wakati muungano wake wa Kenya Kwanza ukiendelea kuyumba kufuatia ushirikiano na Chama cha Pamoja African Alliance (PAA).

Tangu Gavana wa Kilifi, Bw Amason Kingi kuongoza PAA kujiunga na Kenya Kwanza hivi majuzi kumekuwa na mvutano mkali kutoka kwa baadhi ya wanachama wa UDA eneo la Pwani, wakiongozwa na Mbunge wa Malindi, Bi Aisha Jumwa.

Mivutano hiyo imefikia kiwango cha kuwa, Bi Jumwa amemtaka naibu rais kueleza wazi makubaliano yaliyo kati ya PAA na Kenya Kwanza akisema kampeni za UDA zinaathirika.

UDA na PAA zinazozania masuala kama vile usimamizi wa kampeni za urais za Kenya Kwanza, ambapo Dkt Ruto ndiye mwaniaji urais.

Mbali na hayo, mzozo umeibuka kati ya vyama hivyo viwili kuhusu ushindani kati ya wawaniaji wa vyama hivyo katika baadhi ya maeneo.

Kwenye ratiba ya Dkt Ruto, anatarajiwa kuanza rasmi ziara yake kaunti ya Taita Taveta ambapo atakuwa na mkutano katika hoteli ya Voi Wildlife Lodge, kabla kuelekea Kwale kwa mikutano ya hadhara Kinango na Lunga Lunga.

Jumatano, ratiba yake inaonyesha amepangiwa kuwa na mikutano Mombasa kabla aelekee Kilifi.

Baadaye Alhamisi, msafara wake umepangiwa kuelekea Kwale kwa mkutano wa wadau kisha baadaye kufanya mikutano mingine Mombasa.

Ifikapo Ijumaa, ratiba hiyo inaonyesha atatamatisha ziara yake Kaunti za Tana River na Lamu.

Bw Kingi amekuwa akihimiza wapigakura kuchagua wagombeaji wote wa PAA, hali ambayo wafuasi wa Dkt Ruto wanahofia huenda ikagawanya kura za Kenya Kwanza hasa katika Kaunti ya Kilifi.

  • Tags

You can share this post!

MUME KIGONGO: Wataalamu sasa wahusisha ugumba na kansa ya...

SHINA LA UHAI: Kisukari chapofusha idadi kubwa ya wazee Lamu

T L